Polisi Kenya wadaiwa kuwatorosha wenzao wanao tuhumiwa kwa rushwa

Mwandamanaji akipita katika eneo lenye mabango yanayo laani vitendo vya rushwa.

Askari Polisi wa Kenya wanadaiwa wamewasaidia wenzao wawili walio kamatwa kwa shutuma za rushwa kutoroka kizuizini.

Washukiwa hao wawili walikamatwa na kufungwa pingu lakini walitoroshwa na polisi wenzao kutoka kituo cha polisi Kabete ambao walifyatua risasi kadhaa hewani ili kuwawezesha kukimbia, Tume ya maadili na kupambana na rushwa –EACC ilieleza kwenye mtandao wake wa twitter Jumatano.

Maafisa hao walikimbia na shilingi laki moja huku wakiwa wamefungwa pingu.

Polisi hao walifyatua risasi hewani kuwatisha maafisa wanao pambana na rushwa ambao walikuwa wanawashikilia, kitengo cha kupambana na rushwa kimesema.

Maafisa hao wawili ambao wanafanya kazi kwenye idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai, walikamatwa mjini Nairobi Jumatano jioni katika operesheni kali iliyofanywa na maafisa wanaopambana na rushwa.

Tume ya maadili na kupambana na rushwa –EACC ilieleza maafisa hao wakati wakijaribu kuwazingira washukiwa hao wakiwa na hongo ya shilingi laki moja ya Kenya sawa na dola 975, askari hao wanadaiwa waliwasaidia.

.