Mara ya kwanza alikuwa Angola kwa miaka minne. Aliweza kudunduliza fedha, anasema, kwa kufanya kazi saloni ya kusuka nywele pamoja na kutunza.
Baada ya kufanya kazi kwa muda, walisafiri kuelekea Ecuador. Kisha walisafiri kwa basi na kwa boti hadi Colombia. Walikaa huko siku 14 wakivuka hadi eneo la Darien Gap Panama, ikiwa muda mwingi walikuwa katika misitu mikubwa. Walikaa Panama kwa wiki kadhaa, na kisha wiki tatu zaidi huko Costa Rica wakati Julia alikuwa akipata nafuu baada ya kuugua. Kisha walielekea Nicaragua, Honduras, Guatemala.
Hatimaye baada ya mwezi mzima waliokuwa wakisubiri mji wa Acuña, mpakani mwa Marekani na Mexico, walikanyaga katika ardhi ya mchanga kupitia ukanda wa kusini wa Rio Grande. Walikuwa peke yao na walikuwa hawajui kuogelea.
“Tulinuomba Mungu kwanza na kisa tukatumbukia ndani ya maji, Julia anaeleza anavyokumbuka. “Binti yangu alikuwa analia.”
“Mama siwezi…”’ Julia anakumbuka kilio cha mwanawe wakiwa katika maji marefu yanayofika kifuani.
Wakiwa wamefika nusu ya njia, anasema, askari wa Marekani – inawezekana ikawa walinzi wa mpakani – walitupigia kelele, nyoosheni mikono yenu tuwasaidie.’”
“Nilitoa mkono wanisaidie,” Julia anaeleza kumbukumbu yake, “na walituokoa kutoka katika maji yale.”