Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:30

Trump anatarajiwa kutangaza mpango mpya kwa wahamiaji Marekani


Rais wa Marekani, Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump

Mpango utabadilisha malengo ya namna wahamiaji watakavyopatiwa vibali halali ikitoa kipaumbele kwa wenya ujuzi wa juu na watu wasomi wenye ajira au matarajio ya uwekezaji badala ya mahusiano ya kifamilia kwa raia wa Marekani au mahitaji ya kibinadamu

Rais wa Marekani Donald Trump anapanga kutangaza Alhamis pendekezo lake lililosubiriwa kwa muda mrefu la uhamiaji mpango ambao unalengo la kuondoa utaratibu wa wahamiaji kuidhinishwa kutoka mahusiano ya kifamilia na mahitaji ya kibinadamu.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari ofisa mwandamizi wa utawala alieleza kwamba mpango huo utaimarisha usalama wa mpaka na kuunda mfumo utakaozingatia sifa za mtu akisisitiza kwamba ni suala la ushindani wa uwezo wa mtu.

Pendekezo la Trump litaendelea kuweka idadi ya kadi za ukaazi halali Marekani maarufu Green Cards inayotolewa kwa takribani watu milioni 1.1 kila mwaka lakini itabadilisha malengo ya namna wahamiaji watakavyopatiwa ikitoa kipaumbele kwa wenya ujuzi wa juu na watu wasomi wenye ajira au matarajio ya uwekezaji badala ya mahusiano ya kifamilia kwa raia wa Marekani au mahitaji ya kibinadamu.

Mfano wa Visa ya Marekani
Mfano wa Visa ya Marekani

Hivi sasa asilimia 12 ya wahamiaji wanapewa ruhusa ya kuja Marekani kulingana na ujuzi wao na asilimia 66 kwa sababu ya uhusiano wao na familia ambazo tayari zipo Marekani kihalali.

Chini ya mpango huo asilimia 57 ya visa za wahamiaji zitatolewa kwa watu wenye ujuzi au zinatolewa kwenye ajira na asilimia 33 pekee ya watu wenye uhusiano wa kifamilia. Visa zinazotolewa kulingana na mahitaji ya kibinadamu zitapunguzwa kutoka asilimia 22 hadi asilimia 10.

XS
SM
MD
LG