Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:14

Uhamiaji Marekani imeanzisha mpango mpya kuwabana wahamiaji haramu


Polisi wa idara ya uhamiaji na forodha Marekani wakiwa kazini
Polisi wa idara ya uhamiaji na forodha Marekani wakiwa kazini

Kanuni mpya itawaruhusu maafisa wa miji kuwakamata washukiwa wa uhalifu na badala ya kuwaachia washukiwa hao sasa wataipatia ICE saa 48 za ziada kuwafikisha washukiwa kwenye kizuizi cha serikali kuu

Idara ya uhamiaji na forodha ya Marekani-ICE imeanzisha mpango wa ushirikiano kati ya serikali kuu na serikali za wilaya pamoja na majimbo katika ushirikiano ambao utaondowa kanuni za kuwapatia hifadhi wahamiaji wasio na vibali na kuwapatia mamlaka maafisa wa wilaya kuwakamata.

Chini ya mpango huo unaofahamikia kama Warrant Service Officer-WSO uliotangazwa Jumatatu katika wilaya ya Pinellas kwenye jimbo la Florida nchini Marekani. Maafisa wa miji na wilaya wataruhusiwa kuhusika na kuwakamata watu kuhusiana na masuala ya uhamiaji.

Kanuni mpya itawaruhusu maafisa wa miji kuwakamata washukiwa wa uhalifu na badala ya kuwaachia washukiwa hao sasa wataipatia ICE saa 48 za ziada kuwafikisha washukiwa kwenye kizuizi cha serikali kuu.

Kundi moja la haki za kiraia la American Civil Liberties-ACLU lilieleza juhudi hizo ni njama nyingine mpya ya ICE kuwaandikisha polisi wa miji katika ajenda yake ya kuwasafirisha wahamiaji kurudi katika nchi zao za asili kwa njia zisizo za haki.

XS
SM
MD
LG