Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:49

Mdahalo wa Wademokrati : Madai yaliyokosolewa juu ya uchumi, uhamiaji


Seneta Kamala Harris akimsikiliza Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden wakati wa mdahalo Jumatano, Julai 31, 2019.
Seneta Kamala Harris akimsikiliza Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden wakati wa mdahalo Jumatano, Julai 31, 2019.

Baadhi ya wagombea urais wa chama cha Demokratiki walijikita katika kupazia sauti suala lisiloungwa mkono kisiasa kuhusu uhamiaji, uchumi na mengine Jumatano usiku wakati wakipambana kuendelea kuwepo kwenye ushindani katika mdahalo ambao utawachuja wagombea ambao wataondolewa.

Baadhi yao waliendelea kusisitiza katika upotoshaji wa maelezo ya watoto wahamiaji waliokuwa wanazuiliwa mpakani ikiwa moja ya ukatili wa Rais Donald Trump. Wagombea wengine waliendelea kuangaza masuala yenye utata mkubwa, wakati mwengine wakipuuzia masuala yaliyoibuliwa kama ni “hoja za chama cha Republikan” – bila ya kuyajibu.

Wagombea kumi walikuwa katika mdahalo Detroit, kama ilivyokuwa kwa wengine kumi usiku kabla yake. Baada ya hapo, itakuwa vigumu kuweza kuchaguliwa kuingia katika midahalo ijayo na wengine hawatofikia vigezo.

Baadhi ya madai yao yakilinganishwa na ukweli ulivyo

Bill De Blasio,

Meya wa Jiji la New York aliulizwa kwa nini hajawafukuza kazi maafisa wa polisi waliomkaba Eric Garner.

Alisema : “Kwa mara ya kwanza hatusubiri Idara ya sheria ya serikali kuu iliyowaambia jiji la New York kuwa hatuwezi kuendelea na kesi kwa sababu Idara ya Sheria ilikuwa inaendelea na kuwashitaki na miaka imepita na kuendelea kuendeleza maumivu."

Ukweli Ulivyo : Hili jibu ni uongo. Idara ya Sheria haikuzuia uongozi wa jiji kuendelea na kesi hiyo. Idara ya Polisi ya New York iliamua kuchelewesha kuchukua hatua za nidhamu dhidi ya Afisa wa polisi Daniel Pantaleo kwa sababu zao wenyewe.

Cory Booker

Seneta wa New Jersey, alisema kuwa suala la kuondoa sheria ya uhalifu kwa sababu ya uhamiaji haramu katika mipaka : “Inafanya hivyo kupitia mahakama za kiraia inamaana hutahitajia vituo hivi viovu vya kuwazuia wahamiaji ambavyo nimetoka kuvitembelea.

Siyo vile ilivyo. Ni kweli kuwa inawezekana kuwepo punguzo la vituo vya kuwashikilia wahamiaji katika mipaka iwapo hakutakuwa na kufunguliwa kwa makosa ya jinai kwa kuingia nchini kinyume cha sheria. Lakini maafisa wa mpakani bado watahitajika kushughulikia kuingia kwa watu wanaopita mpakani na hilo linaweza kupelekea watu hao kuzuiliwa, katika vizuizi ambavyo Wademokrat wanaviita ni kinyume cha ubinadamu.

Kamala Harris

Seneta wa California alisema : “Wafanyakazi katika viwanda vya magari tunatarajia, pengine, mamia kwa maelfu watapoteza ajira ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Ukweli ulivyo: Utabiri huu hasi una dosari. Viwanda vya magari haukabiliwi na hatari ya wazi ya kuharibikiwa.

Hilo lingeweza kutokea – kwa hali mbaya zaidi – iwapo Trump angetekeleza tishio la kuanzisha ushuru mpya na sera nyengine ambazo zingeathiri viwanda vya magari. Lakini hakufanya hilo.

Harris amekuwa akitoa tafiti ya Kituo cha Utafiti cha Utengenezaji magari ya 2018, iliyokuwa inafanya makadirio ya ajira kupotea nchini Marekani.

Hivi sasa nchini Marekani, tunawatu wastaafu ambao kila siku - mamilioni ya wastaafu - wanatumia huduma ya afya ya Medicare."

Ukweli Ulivyo : Ni zaidi ya watu 10,000 kwa siku wanaofikia miaka 65 na watastahili kuwa na huduma ya Medicae, ambayo inawawezesha kulazwa, kumuona daktari, kuandikiwa dawa na huduma nyingine.
Medicare inawafikia zaidi ya watu milioni 60, wakiwemo walemavu wa umri wowote.
Makamu wa Rais wa Marekani wa zamani, Joe Biden alisema : “Ni lazima baadhi ya watendaji hawa wa makampuni ya bima wanaopinga mpango wangu wafungwe jela kwa madawa yenye thamani ya dola bilioni 9 yaliyosababisha madhara wanaowauzia watu.”

Ukweli Ulivyo : Makamu wa rais mstaafu lazima alikuwa anakusudia watendaji wa makampuni ya madawa, kwa kuwa makampuni ya bima yanalipa kwa ajili ya watu kupatiwa dawa – wao siyo wanaouza.

Michael Bennet,

Seneta kutoka Colorado, katika ujumbe wa moja kwa moja kwa Trump alisema: “Watoto wanatakiwa kuwa madarasani na siyo katika vizuizi.”

Ukweli Ulivyo: Vizuizi hivi wanakozuiliwa wahamiaji watoto katika mpaka vilijengwa na kutumiwa na Rais Barack Obama. Uongozi wa Trump imeendelea kuvitumia. Alichokuwa anakusudia ni vizuizi ndani ya majengo ya mpakani ambako wahamiaji wamewekwa kwa muda, wakitenganishwa kwa jinsia na umri.

Ni kweli kuwa uongozi wa Trump uliwatenganisha angalau watoto wahamiaji 2,700 kutoka kwa wazazi wao chini ya sera iliyositishwa kwa muda ya "hakuna simile." Obama hakufanya kuwa desturi kwa familia za wahamiaji waliokuwa wanashikiliwa mpakani kutenganishwa.

XS
SM
MD
LG