Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 19:44

Wagombea mchanganyiko Wademokrati kupambana na Trump


Seneta Elizabeth Warren
Seneta Elizabeth Warren

Ushiriki wa Chama cha Demokrat katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais 2020 unaendelea kuongezeka wiki hii kwa kujitokeza rasmi Seneta wa Jimbo la Minnesota Amy Klabuchar na Seneta Elizabeth Warren wa Massachusetts.

Lakini kura za maoni mpya zinatoa bishara njema kwa wagombea hao kwa kutojitokeza katika kinyang’anyiro hicho, Seneta wa Jimbo la Vermont Bernie Sanders, ambaye aligombea mwaka 2016, na Makamu wa Rais mstaafu Joe Biden.

Kura za maoni zilizofanywa na taasisi ya Morning Consult imegundua kuwa Biden alikuwa akiongoza katika maeneo ya Wademokrat akiungwa mkono kwa asilimia 29, akifuatiwa na Sanders ambaye anaungwa mkono kwa asilimia 22 na Seneta wa Jimbo la California Kamala Harris akiwa nafasi ya tatu na kuungwa mkono kwa asilimia 13.

Hii ni bishara njema kwa Harris, ambaye kati ya wagombea Wademokrat kadhaa wapya ambao wamezindua kampeni zao katika siku za karibuni, tayari ameonyesha kuwa ni kivutio katika kura za maoni kadhaa zilizofanyika hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG