Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kila mmoja amesema nchi zao ziko tayari kumkubali Juan Guaido kama kiongozi wa Venezuela.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani Martina Fietz amesema kupitia ujumbe wa Twitter kuwa Ujerumani pia itamtambua Guaido iwapo Venezuela itashindwa kufanya uchaguzi mpya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amemchagua mzoefu wa sera za kigeni Elliott Abrams kuwa mjumbe maalum atayeshughulikia masuala ya sera ya Marekani juu ya Venezuela, ambaye amepewa jukumu la kusaidia “kurejesha demokrasia katika taifa hilo la Amerika Kusini.
Tamko la Pompeo alilolitoa Ijumaa mchana mjini Washington, kabla ya kikao maalum cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana Jumamosi.
Pompeo amesema Abrams atasafiri pamoja naye kuhudhuria mkutano huo, ambao uliitishwa na Marekani.