Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:19

Venezuela yailaumu Marekani jaribio la kuuwawa Maduro


Waziri wa Mambo ya Ndani na Sheria wa Venezuela's Nestor Reverol akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya jaribio la kumuuwa rais huko mjini Caracas, Venezuela Agosti 5, 2018.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Sheria wa Venezuela's Nestor Reverol akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya jaribio la kumuuwa rais huko mjini Caracas, Venezuela Agosti 5, 2018.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema kwamba anaamini kuwa Marekani na Colombia ndio waliohusika na jaribio la kumuuwa lililotokea mwisho mwa wiki.

Mshauri wa usalama wa taifa nchini Marekani John Bolton hata hivyo amekanusha madai ya Marekani kuhusika katika jaribio hilo.

Katika hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini Venezuela, Rais Maduro amesema kwamba kila ishara inaonyesha kwamba ni jirani wa Venezuela, Colombia, ndio mhusika mkuu wa jaribio hilo la kumuua na kuongezea kwamba Mungu, watu wa Venezuela na wanajeshi wake ndio waliomuokoa.

"Hiyo ndege yenye mabomu ilikuwa imenilenga mimi lakini kinga ya upendo iliniokoa. najua nitaishi miaka mingi zaidi," amesema Maduro.

Ndege yenye vilipuzi na isiyoruka na rubani, vililipuka majira ya saa kumi na moja dakika 41 Jumamosi jioni, wakati Maduro alipokuwa akihutubia umati wa maelfu ya wanajeshi katika uwanja wa mji mkuu wa Caracas.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP, Rais Maduro hakupata majeraha yoyote lakini wanajeshi saba walijeruhiwa.

Maduro amesema kwamba hana shaka kwamba Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, anahusika na shambulizi hilo.

Shirika la habari la AFP linamnukuu afisa wa serikali ya Colombia akisema kwamba shutuma hizo dhidi ya Rais Santos "hazina msingi wowote"

Maduro amesema kuwa uchunguzi wa awali "unaonyesha kwamba wanaofadhili watu wanaotaka kumuuwa wanaishi katika jimbo la Florida nchini Marekani. "Ni matumaini yangu kwamba rais Donald Trump yupo tayari kupigana na hawa magaidi"

Kiongozi huyo wa Venezuela amesema kwamba watu kadhaa wanaopanga njama ya kumuua wamekamatwa, lakini hakutoa taarifa zaidi.

shambulizi lilitokea wakati Maduro alikuwa akizungumzia kuhusu uchumi wa Venezuela. video zinaonyesha Maduro na wengine wakiwa wameduwaa baada ya sauti ya milipuko mikubwa kadhaa kusikika. mda mfupi baadaye, video inaonyesha wanajeshi wakitafuta mahali pa kujikinga.

nchi ya Venezuela imekumbwa na mgogoro wa kisiasa kwa muda mrefu. Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, uchumi wa nchi ya Venezuela umeporomoka, mfumuko wa bei ukikaribia kufika asilimia mia mojamwaka 2018, huku nchi hiyo ikikumbwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu pamoja na uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu.

Katika siku za hivi karibuni, maelfu ya raia wa Venezuela wamelazimika kukimbilia nchi jirani kutokana na hali ngumu ya maisha nchini mwao.

Maduro alichaguliwa kuwa rais wa Venezuela mnamo mwezi Mei 2018 kutawala kwa mhula wa miaka sita katika uchaguzi ambao wanasiasa wa upinzani na waangalizi wa kimataifa walikataa matokeo yake, kwa msingi kwamba ulikumbwa na udanganyifu katika zoezi la kuhesabu kura.


XS
SM
MD
LG