Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:39

UN yashauri kufanyike mazungumzo mgogoro wa Venezuela


Balozi wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
Balozi wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametaka kuwepo mazungumzo kupunguza mvutano unaoendelea Venezuela, akisema kuwa “ mgogoro huu unaweza kwenda kombo na kushinidikana kudhibitiwa na kuleta maafa makubwa.”

Bachelet pia ametaka uchunguzi huru ufanyike juu ya ripoti zinazoeleza kuwa vyombo vya usalama vya Venezuela viliuwa watu 20 na kuwakamata zaidi ya waandamanaji 350 wiki hii.

Rais wa Marekani Donald Trump amemuonya waziwazi Maduro Alhamisi kuwa “hatua zote zinazoweza kuchukuliwa ziko mezani” iwapo hapatakuwa na kukabidhiana madaraka kwa njia ya demokrasia katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Guaido, spika wa Bunge la Venezuela, alijitangaza mwenyewe kuwa rais wa muda siku moja kabla, wakati wa maandamano makubwa.

Sakata hilo katika nchi hiyo ya Amerika Kusini lilizidi kuongezeka Jumatano baada ya Rais Maduro kutangaza kuwa anasitisha mahusiano ya kidiplomasia na Marekani, akijibu tangazo la Rais Donald Trump kwamba anamtambua rasmi Guaido kuwa ni Rais wa muda wa Venezuela.

Maduro ameamrisha kuwa wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Marekani waondoke nchini katika kipindi cha masaa 72. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, hata hivyo, amesema Maduro hana tena madaraka ya kutoa amri hiyo.

XS
SM
MD
LG