Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:00

Wademokrat wadhibiti baraza la wawakilishi


Nancy Pelosi
Nancy Pelosi

Wademokrat wamechukua udhibiti wa baraza la wawakilishi huku warepublikan wakiongeza nguvu yao katika udhibiti wa baraza la seneti katika bunge la marekani baada ya uchaguzi wa katikati ya awamu.

Mpaka kufika Jumatano asubuhi baada ya upigaji kura Jumanne wademokrat walikuwa wanaelekea kushinda kwa viti vipatavyo 26 katika baraza la wawakilishi ambavyo vilikuwa vinashikiliwa na warepublikan. Hadi hesabu ya mwisho itakapotoka wademokrat huenda wakawa na viti 230 katika baraza lenye wajumbe 435.

Katika baraza la seneti, Warepublikan waliwashinda kirahisi wademokrat waliokuwa wakishikilia viti katika majimbo ya Indiana, Missouri na north Dakota. Kwa ushindi huo warepublikan wameongeza nguvu yao katika kudhibiti baraza la seneti kwa kuwa na viti zaidi ya viwili vya ziada walivyokuwa navyo kabla ya uchaguzi.

Miongoni mwa washindi katika uchaguzi wa jumanne ni pamoja na wabunge wa mara ya kwanza ikiwa ni pamoja na wanawake wawili waislamu, mmarekani wa asili hapa nchini. Baraza la wawakilishi litakuwa na wanawake 100 litakapoapishwa januari mosi.

Licha ya kupoteza baraza la wawakilishi rais Donald trump alitoa ujumbe wa twitter kujipongeza mwenyewe Jumatano asubuhi akisema amepata salamu nyingi za pongezi kutoka kwa marafiki ikiwa ni pamoja na kutoka nchi za nje.

XS
SM
MD
LG