Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:12

Uchaguzi 2018: Historia ya uchaguzi wa katikati ya awamu Marekani


Sehemu ya jengo la Bunge la Congress Marekani
Sehemu ya jengo la Bunge la Congress Marekani

Wakati uchaguzi wa kila baada ya miaka miwili wa wawakilishi 435 wa bunge la Congress na theluthi moja ya Baraza la Seneti huwa unakosa mvuto na vuguvugu la wapiga kura kinyume na ilivyo wakati wa uchaguzi wa rais kila baada ya miaka minne, uchaguzi wa katikati ya awamu unaathari kubwa katika muundo na muelekeo wa bunge la Congress.

“Bunge la Congress linaundwa na wawakilishi wanaochaguliwa kila baada ya miaka miwili na watu wa majimbo mbalimbali.” – kwa mujibu wa Katiba ya Marekani.

Hivi sasa kampeni zinaendelea kote nchini kabla ya uchaguzi wa wabunge na maseneta, wa katikati ya awamu, ambao utafikia kilele chake Jumanne Novemba 06, 2018.

Nafasi ya rais katika chaguzi hizo

Uchaguzi wa Bunge wa katikati ya awamu unaonekana mara nyingi kama ni kura ya maoni juu ya rais aliyeko madarakani.

Marais wengi wamekuja kutambua kuwa umaarufu wao umepungua baada ya miaka miwili ya kutumikia wadhifa huo, na hilo mara nyingi linafanya wapiga kura wanaomuunga mkono rais kutojitokeza wakati wa uchaguzi wa katikati ya awamu.

Wakati huu chama cha upinzani huwa kinamuelekeo wa kuwa chenye nguvu katikati ya awamu, na kihistoria hilo limesababisha chama cha rais kupoteza viti katika bunge. Tangu vita vya wenyewe kwa wenye nchini Marekani mwaka 1860, chama cha rais kimepoteza nafasi yake katika chaguzi za katikati ya awamu 36 kati 39.

Wastani wa wabunge kupoteza nafasi zao wakati rais anapokuwa anaungwa mkono kwa asilimia zaidi ya 50 ni viti 14.

Wastani wa wabunge kupoteza nafasi zao wakati rais anapokuwa anaungwa mkono chini ya asilimia 50 tangu mwaka 1970 : ni viti 33.

Katika chaguzi za katikati ya awamu zilizokuwa na matokeo mabaya sana tangu Vita vya Pili vya Dunia : Wademokrat walipoteza viti 63 katika Bunge la Congress katika awamu ya Rais Barack Obama mwaka 2010 na viti 52 wakati wa kipindi cha Rais Bill Clinton mwaka 1994.

Warepublikan walipoteza viti 30 katika Bunge la Congress chini ya uongozi wa Rais George W. Bush mwaka 2006 na viti 48 vya wawakilishi wakati wa uongozi wa Rais Gerald Ford mwaka 1974.

Waipiku historia

Wademokrat walipata viti vitano vya Bunge la Congress mwaka 1998 kufuatia hatua ya kutaka kumuondoa Rais Clinton madarakani iliyo ongozwa na Warepublikan.

Warepublikan pia walipata viti vinane katika Bunge na viti viwili katika Baraza la Seneti chini ya uongozi wa George W. Bush mwaka 2002, uchaguzi wa kwanza tangu shambulizi la kigaidi litokee Septemba 11, 2001.

Idadi ya wanaojitokeza kupiga kura

Wakati wa uchaguzi wa urais, wastani wa wapiga kura wanaojitokeza ni kati ya asilimia 50 na 60 ya wanaostahili kupiga kura.

Idadi hiyo hupungua kufikia asilimia 40 wakati wa uchaguzi wa katikati ya awamu wa Bunge la Congress.

Mwaka 2014 waliojitokeza kupiga kura : asilimia 36.4, idadi ya chini kabisa tangu mwaka 1942.

Mwaka 2016 waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa rais : asilimia 58.1.

XS
SM
MD
LG