Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:27

Mdemokrat Doug Jones ashinda uchaguzi wa seneta Alabama


Seneta mteule wa Alabama, Doug Jones (kulia).
Seneta mteule wa Alabama, Doug Jones (kulia).

Mdemocrat Doug Jones Jumanne usiku alishinda uchaguzi maalum wa kujaza nafasi katika baraza la Senate la Marekani ili kuliwakilisha jimbo la kusini la Alabama.

Baada ya kipindi cha kampeni kali, wapiga kura walimuunga mkono Jones dhidi ya Mrepublican Roy Moore.

Matokeo hayo yana maana kwamba mwezi Januari, Jones ataapishwa, na wingi wa Republican katika baraza la Senate utapungua na kuwa na viti 51 dhidi ya 49 jambo ambalo litafanya iwe vigumu zaidi kwa Rais Donald Trump kupitisha ajenda zake.

Muda wa kuhudumu katika senate ni miaka sita, lakini Jones ataijaza nafasi hiyo kwa muda uliobaki wa miaka mitatu ambapo awali kiti hicho kilikuwa kinashikiliwa na Jeff Sessions kabla ya kujiuzulu ili kuwa mwanasheria mkuu katika utawala wa Trump.

Jones ni Mdemocrat wa kwanza kutoka Alabama kushinda kiti cha senate tangu mwaka 1992.

Moore alikuwa akiungwa mkono na Trump, lakini alikabiliwa na upinzani kutoka kwa viongozi wengine wa Republican. Alishutumiwa kwa vitendo vya manyanyaso ya ngono katika miaka ya 1970 wakati wanawake kadhaa ambao walikuwa vijana wakati na yeye alikuwa katika umri wa miaka ya 30.

Moore mara kwa mara amekanusha shutuma hizo na kuziita ni za “kuchukiza.” Lakini awali alikiri kuwa na mahusiano na wasichana wadogo, wakati alipokuwa mwanasheria mkuu, kabla ya kukanusha kuwa hawafahamu wale wanaomshutumu.

Mwanamke mmoja alimuita Moore ni muongo.

Jumanne asubuhi, Moore akiwa amevaa kofia ya ‘cowboy’ aliwasili akiwa amepanda farasi kwenda kupiga kura yake huko Gallant, mji mdogo uliopo kaskazini mashariki mwa Alabama.

XS
SM
MD
LG