Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:40

Trump, Obama wachuwana katika kampeni za uchaguzi wa Novemba


Rais Donald Trump na Rais Barack Obama
Rais Donald Trump na Rais Barack Obama

Kwa Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama, inaweza ikawa ni fursa nyingine ya kukutana na wanachama wenzake.Trump and Obama Face Off in Midterm Battle

Obama ameanza kuzunguka katika kampeni kwa niaba ya Wademokrat kabla ya uchaguzi wa wabunge na maseneta, wa katikati ya awamu, Novemba, na kuanzisha kile kinachoelekea kuwa ni mapambano anayo wakilisha chama chake dhidi ya mrithi wake, Rais Donald Trump.

Rais Trump

Trump tayari amekuwa akiendesha kampeni hiyo kwa niaba ya Warepublikan, akiwa ana amini kuwa juhudi za nguvu za kampeni katika majimbo yenye kuungwa mkono na Warepublikan utalinda maslahi ya Warepulikan walio wengi katika Baraza la Seneti na Bunge.

Hatua ya kwanza ya Obama katika kampeni za kutafuta wabunge 2018 zimefanyika katika Chuo Kikuu cha Illinois ambapo amehimiza vijana Wademokrat kuendeleza mapambano ya kampeni hizo katika masuala ya haki za jamii na za kiuchumi.

“Kila wakati tunapokuwa tumekaribia kufikia misingi hiyo, kuna mtu yuko mahali fulani ametuzuia,” amesema Obama. “Haikuanza na Donald Trump. Yeye ni dalili ya tatizo na siyo mwenye kusababisha hili. Anajaribu kutumia fursa iliyopo ya hasira zinazochochewa na wanasiasa kwa miaka mingi.”

Watakiwa wakapige kura

Obama pia amefanya kampeni huko California kwa niaba ya wagombea kadhaa wa nafasi za Bunge kutoka chama cha Demokrat, ambapo amehimiza wanaharakati kujitokeza na kupiga kura Novemba 2018.

“Wakati tukiacha kushiriki katika kupiga kura, ikiwa hatuna umakini, iwapo hatuchukuwi hatua, sauti nyingine zinajaza nafasi hiyo iliyoko wazi,” Obama ameuambia umati mkubwa wa Wademokrat uliokusanyika Anaheim. Lakini habari njema ni kuwa katika kipindi cha miezi miwili, tutapata nafasi ya kurudisha busara katika siasa zetu.”

Hivi sasa Obama amejikuta analazimika kuingia katika ushindani na mtu ambaye ni mrithi wake, Rais Trump, ambaye ameahidi kuondoa mengi kati ya yale aliyo yafanya wakati akiwa rais.

Trump awatahadharisha Warepublikan

Kwa upande wake, Trump amekuwa na ana hamasa ya kwenda kufanya kampeni na ameahidi kutumia juhudi zote kuhamasisha wapiga kura Warepublikan ili kuhakikisha wanaendelea kuwa ni waliowengi mwezi Novemba katika bunge.

Trump pia anajenga hofu kati ya wafuasi wa chama cha Republikan kuwa Wademokrat wakishinda uchaguzi wa Bunge Novemba itapelekea yeye kuondolewa madarakani.


XS
SM
MD
LG