Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 19:53

Pelosi achaguliwa tena Spika wa Bunge la Marekani


Nancy Pelosi
Nancy Pelosi

Nancy Pelosi ameapishwa Alhamisi na kuendelea kuwa mwanamke mwenye nguvu za ushawishi zaidi wa kisiasa katika historia ya siasa za Marekani, akianza na zama mpya za utawala wa serikali ya Marekani uliogawanyika na kuanzisha upinzani wa kisiasa wenye nguvu dhidi ya Rais Donald Trump.

Historia ya Pelosi ya kurejea mara ya pili kuongoza Wademokrati walio wengi kama spika wa Baraza la Wawakilishi inaingia katika kumbukumbu kuwa kwa mara ya pili kwa kipindi cha nusu karne kwa spika kurejea na kutumikia wadhifa huo.

Pelosi ameendelea kuwa shupavu katika kukabiliana na changamoto za kuwa mwanamke katika medani ya siasa – na bado ni mwanamke pekee kuwa spika—atatoa muelekeo wake wakati akigeukia mgogoro uliokuwepo kwa kufungwa baadhi ya ofisi za serikali ambazo zimefungwa kwa amri ya Rais Trump.

Wademokrat katika Bunge watapitisha miswada sita ya kuruhusu matumizi kwa idara za serikali hadi Septemba mwaka huu.

Muswada mewngine utaipatia fedha Wizara ya Mambo ya Ndani – Idara itakayo simamia fedha za ujenzi wa Ukuta kati ya Marekani na Mexico – zitatolewa kufikia Februari 8, 2018.

XS
SM
MD
LG