Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:42

Pelosi amtuhumu Trump kwa kutosimamia jukumu lake la kikatiba


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Kiongozi wa Wabunge wa Demokrat Nancy Pelosi amemtuhumu Trump kwa kutosimamia jukumu lake la kikatiba kutokana na hatua yake ya kuruhusu waraka wa siri ya juu kabisa kutolewa kwa umma na kupotoshwa kwa taarifa za upelelezi.

“Kitendo cha yeye kutolinda vyanzo vya habari za upelelezi na utaratibu mzima wa kukusanya habari hizo, amempelekea shada la maua rafiki yake Putin (Rais wa Russia),” Pelosi amesema katika tamko lake.

Rais Trump Ijumaa asubuhi ameruhusu waraka wa siri kuwekwa wazi kwa umma, na kuupeleka kwa kamati ya Bunge, kitendo ambacho kimewakasirisha upinzani wa Demokrat nchini Marekani.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Wademokrat ambao wameuona waraka huo ambao ni maarufu kama “Waraka wa Nunes”, na kuonyesha namna waraka huo ulivyochagua siri za kumkandamiza Rod Rosenstein, naibu mwanasheria mkuu, na kumfanya kuwa ndiye aliyekuja na njama za Shirika la Upelelezi FBI kumuangaza aliyekuwa msaidizi wa Trump Carter Page.

Trump anaona waraka huo ni muhimu katika kuleta mabadiliko anayatoka katika idara ya Sheria, gazeti la Washington Post liliripoti Alhamisi, zikinukuu chanzo cha habari cha ikulu ya White House.

Rosenstein anasimamia upelelelezi unaofanywa na mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller juu ya madai ya hujuma iliyofanywa kati ya timu ya kampeni ya Trump na Russia. Kuondolewa kwake kutapelekea usimamzi huo wa Mueller kwenda mikononi mwa mtu mwengine na kunaweza kuwa ni tishio kwa uchunguzi huo.

XS
SM
MD
LG