Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:35

Bunge jipya la Marekani laapishwa Alhamisi


Wabunge wapya wa Bunge la Marekani wakiwa nje ya bunge hilo, Washington, Novemba 14, 2018.
Wabunge wapya wa Bunge la Marekani wakiwa nje ya bunge hilo, Washington, Novemba 14, 2018.

Utawala wa serikali ya Marekani uliyo gawanyika unarejea kazini Marekani Alhamisi wakati Bunge jipya la Marekani likiapishwa.

Baada ya miaka miwili ambapo Warepublikan wamekuwa wakiidhibiti White House, Baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi, Wademokrat ndio walio wengi hivi sasa katika Baraza la Wawakilishi.

Haya ni matokeo ya uchaguzi wa katikati ya awamu ambapo Wademokrat waliongeza wawakilishi wao na kushikilia viti 235 katika Bunge lenye viti 435 wakati idadi mpya itakapoanza shughuli zake. Warepublikan walipata viti viwili katika Baraza la Seneti na hivi sasa ni walio wengi kwa viti 53-47.

Mwakilishi Nancy Pelosi kutoka California anategemewa kuchaguliwa kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, na atarejea katika wadhifa ambao aliushikilia kuanzia mwaka 2007 mpaka 2011. Yeye ni mwanamke pekee ambaye amewahi kuwa spika wa baraza hilo, na iwapo atachaguliwa tena atakuwa mtu wa kwanza kwa zaidi ya miaka 60 kuchukuwa tena nafasi hiyo baada ya chama chake kupoteza idadi ya walio wengi na baadaye kuweza kurudi kwa ushindi wa kuwa na idadi ya walio wengi.

Baadhi ya Wademokrat walionyesha nia yao ya kupata viongozi wapya katika chama hicho, na Pelosi amekubali kutumikia kipindi cha miaka minne tu kama spika ikiwa ndio njia ya kupata kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya wawakilishi wa chama chake kutumikia tena wadhifa huo.

Bunge jipya ni lenye kuleta watu wa mchanganyiko mbalimbali kuliko mabunge yote yaliyopita katika historia.

XS
SM
MD
LG