Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:03

Wanawake Waislam Marekani waweka historia uchaguzi - Baraza la Wawakilishi


Washindi wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa katikati ya awamu Ilhan Omar (kushoto) na Rashida Tlaib (kulia).
Washindi wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa katikati ya awamu Ilhan Omar (kushoto) na Rashida Tlaib (kulia).

Uchaguzi wa katikati ya awamu 2018 nchini Marekani umeweka historia, moja wapo ikiwa kuchaguliwa kwa wanawake wa kwanza wa Kiislam, Ihlan Omar na Rashida Tlaib, Wademokrati kuingia katika Baraza la Wawakilishi.

Omar mwenye umri wa miaka 36 alikuja Minnesota miaka 20 iliyopita baada ya kukimbia vita nchini Somalia, na kukaa katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya kwa miaka minne.

Mwakilishi huyo amemshinda kirahisi mpinzani wake Mrepublican Jennifer Zielinski katika jimbo ambalo lina wademokrat wengi.

Omar aahidi kupambana na Trump

Omar ameahidi baada ya kuchaguliwa kupambana na sera za Rais Donald Trump aliyekuwa ameanzisha sera za kuzuia watu kuja Marekani.

“Sera hizi ni za hatari, nadhani ziko kinyume kabisa na thamini za taifa hili….natumai kwenda Washington na watu ambao tuna mawazo sawa…..na kumwajibisha kwa sera anazoleta za hofu na mgawanyiko,” amesema Mwakilishi huyo.

"Mabadiliko ya kutumia siasa kama chombo cha kuleta mafanikio ndio ambayo yamenipa nguvu ya kuingia katika siasa na kupanua demokrasia yetu imfikie kila mtu, na kugombea kiti hiki ili kuleta sera ambazo zitasaidia watu," amesema.

Mhamiaji mwenye asili ya Somalia

Ilhan Omari mhamiaji mwenye asili ya Somalia ametokea Afrika kuingia congress.

Miongoni mwa chaguzi zinazoangaliwa kwa karibu sana na wahamiaji hapa Marekanini ule wa jimbo moja la uchaguzi la Minnesota.

Ilhan omar aliweka historia mwaka 2016 alipoingia katika baraza la wawakilishi la jimbo la Minnesota na kuwa mmarekani-msomali wa kwanza kuwa mbunge katika jimbo hilo, ambalo lina idadi kubwa ya jamii wa wamarekani-wasomali.

Katika mwaka 2018 ambapo idadi ya wanawake wanaogombania viti wameweka rekodi, omar amewatia moyo wanawake wengi Waislam katika taifa hili, ikiwa ni pamoja na Hodan Hassan ambaye anagombania kiti katika baraza la wawakilishi la jimbo na Minnesota.

Mwanamke mwengine Muislam

Pia katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi wa katikati ya awamu mwanamke mwingine Muislamu Rashida Tlaib kutoka Detroit, naye ameshinda kuingia katika baraza la wawakilishi.

Mwandishi wa VOA anaripoti kuwa sababu ya wanawake wengi kugombea ni mbili, kwanza ni ile #METOO vuguvugu la kupinga unyanyasaji wa kingono, na pili ni Donald trump ambaye alichaguliwa akiwa na tabia na anaendelea na tabia ya kutoheshimu wanawake , kwa sababu hizo mbili zimepelekea wanawake wengi kutaka mabadiliko na njia moja ni kugombania ofisi za umma.

Uchaguzi huu wa katikati ya awamu unafanyika wakati Marekani iko katika mgawanyiko mkubwa wa kisiasa. Wachambuzi wanasema kuwa wanasiasa wanatakiwa kuleta umoja na kueneza ujumbe wa kuunganisha watu.

XS
SM
MD
LG