Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:19

Spika ayatupilia mbali madai ya Trump


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Spika wa Bunge la Marekani Paul Ryan Jumatano ameyakataa madai ya Rais Donald Trump kuwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai walimpeleka “jasusi” katika kampeni yake ya 2016.

Trump amekuwa akikiita kitendo cha FBI kumtumia jasusi ambaye alipeleka mazungumzo yake aliyokuwa akifanya na washirika wake wa kampeni kuwa ni “Spygate”

Rais alidai kuwa FBI ilikuwa imemtuma jasusi wakati wa kampeni yake katika juhudi ya kumuangusha katika kinyang’anyiro cha urais.

Vyombo vya habari vilimtambulisha mtu huyo kuwa ni Stefan Halper, Profesa aliyezaliwa Marekani anayefanya kazi Chuo Kikuu cha Cambridge Uingereza.

Ryan, ambaye ni kiongozi wa Republikan chama chenye wabunge wengi, hivi karibuni alizipitia taarifa za siri zinazoelezea kitendo cha FBI kumtumia jasusi kama ni sehemu ya upelelezi dhidi ya kitendo cha Russia kuingilia uchaguzi.

Ryan told reporters that he agreed with the assessment of another key Republican lawmaker, Congressman Trey Gowdy, who reviewed documents in the case and concluded that the FBI did nothing wrong.

Ryan amewaambia waandishi wa habari kuwa anakubaliana na tathmini iliyofanywa na mbunge muhimu wa chama cha Republikan, Trey Gowdy alizipitia nyaraka hizo za siri na kutoa majumuisho kwamba FBI haikufanya kosa lolote.

XS
SM
MD
LG