Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:58

Mazungumzo ya kufungua serikali kuu Marekani hayajatoa ishara njema


Rais Trump kabla hajakutana na wabunge alisema serikali kuu itaendelea kufungwa hata kama itachukua muda na aliliambia baraza lake la mawaziri “huwenda ikachukua muda mrefu au muda mfupi.

Kiongozi wa warepublican katika bunge Kevin McCarthy alisema Rais Donald Trump aliwakaribisha viongozi wa bunge kurudi White House siku ya ijumaa kwa mazungumzo zaidi juu ya kufungwa kwa serikali kuu.

Trumpa anataka apatiwe dola bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico. Wa-Democrat wanakataa kutenga kiwango hicho. Mkutano wa Jumatano kati ya Rais Trump na wademocrat na warepublican ulimalizika bila ishara ya mafanikio licha ya rais kuwa tayari kuendelea na mazungumzo.

Kevin McCarthy akiwa Washington, Jan. 2, 2019.
Kevin McCarthy akiwa Washington, Jan. 2, 2019.

McCarthy aliwaambia waandishi wa habari “Tunafahamu tuna changamoto kwenye mpaka. Tunataka kutatua suala hilo. Tunataka kuhakikisha tunafungua serikali na ninafikiri mwisho wa siku rais nilivyomsikiliza anataka kutatua suala hili pia”.

Kabla ya kukutana na wabunge Rais Trump alisema serikali kuu itaendelea kufungwa hata kama itachukua muda. Rais Trump aliliambia baraza lake la mawaziri, “huwenda ikachukua muda mrefu au muda mfupi.

XS
SM
MD
LG