Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:10

Wabunge Marekani wanajadili kufungwa serikali kuu


Kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali kuu Marekani kunakaribia kutimiza wiki moja lakini mivutano bado inaendelea na fursa inaonekana finyu ya kupitisha bajeti anayoitaka Rais Trump kwa ajili ya fedha za kujenga ukuta

Bunge la Marekani litakuwa na fursa ya kumaliza kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali kuu baadae Alhamis wakati wabunge wanarudi kutoka likizo fupi ya Christmas. Lakini fursa hiyo inaonekana finyu ya kupitisha mswaada wa matumizi ambao bunge na Rais Trump wanaweza kuunga mkono.

Kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali kuu Marekani kunakaribia kutimiza wiki moja lakini mivutano bado inaendelea. Rais Trump anataka apewe mabilioni ya dola kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico. Wademocrat wanaunga mkono fedha kwa ajili ya ulinzi wa mpakani lakini sio kwa ajili ya ujenzi wa ukuta.

Seneta Mitch McConnell, wa jimbo la Kentucky kwa tiketi ya Republican
Seneta Mitch McConnell, wa jimbo la Kentucky kwa tiketi ya Republican

Kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti mrepublican Mitch McConnell anasema hakutakuwa na upigaji kura hadi Trump na wademocrat watakapokubaliana juu ya bajetia ya matumizi.

White House inaonesha ishara ya kukubaliana na kiwango cha fedha kilichohitajika kwa ujenzi wa ukuta, lakini Rais Trump hajapendekeza mageuzi yeyote yanayohusiana na uhamiaji ambayo yaliwapatia ushindi wademocrat kwa kuongeza fedha za usalama wa mpakani katika siku za nyuma.

Wademocrat hawatetereki katika upinzani wa kufadhili ujenzi wa ukuta wakiamini nafasi itakuwa nzuri katika majadiliano wakati baraza jipya la wawakilishi lenye wademocrat walio wengi litakapochukua udhibiti bungeni mwanzoni mwa Januari 2019.

XS
SM
MD
LG