Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:14

Serikali kuu Marekani bado imefungwa


Jengo la bunge la Marekani mjini Washington, Dec. 22, 2018.
Jengo la bunge la Marekani mjini Washington, Dec. 22, 2018.

Rais Trump alieleza akiwa White House siwezi kusema lini serikali itafunguliwa. Naweza kusema serikali itafunguliwa pale tutakapokuwa na fedha ya ukuta au uzio chochote wanachokiita

Kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali kuu ya Marekani hakuonekani kuwa suluhisho la karibuni litapatikana huku Rais Donald Trump akisisitiza siku ya Jumanne kuwa serikali itaendelea kufungwa mpaka madai yake ya kutaka fedha za ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico yameridhiwa.

"Siwezi kusema lini serikali itafunguliwa. Naweza kusema itafunguliwa pale tutakapokuwa na fedha ya ukuta, uzio chochote wanachokiita" Trump alisema kwenye ofisi yake huko White House baada ya kuzungumza na wanajeshi wa Marekani kwa njia ya video walio kwenye mataifa ya nje.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Trump alidai kuwa maelfu ya wafanyakazi wa serikali ambao wako nyumbani kutokana na serikali kuu kufungwa pia wanataka ukuta ujengwe licha ya ukosefu wa ushahidi wa kuunga mkono madai yake.

Jumatatu Trump alisema wademocrat lazima wamalize tatizo hili wakati viongozi wa Democrat katika bunge wamemlaumu Trump kwa kuitumbukiza nchi katika vurugu.

XS
SM
MD
LG