Israeli yaendeleza operesheni zake za kijeshi kabla ya moja ya sikukuu kubwa

Wapalestina wakiomboleza vifo vya ndugu zao waliouawa katika mashambulizi ya mabomu yanayofanywa na Israeli huko Ukanda wa Gaza nje ya jumba la kuhifadhia maiti huko Khan Younis Dec. 24, 2023.

Israel iliendelea na operesheni zake za kijeshi dhidi ya Hamas na washirika wake kabla ya moja ya sikukuu kubwa za kikritso.

Lakini nchini Marekani, maafisa wanaonya kuhusu kuongezeka kwa vitisho kutokana na mzozo huko Gaza.

Mkesha wa Krismas huko Gaza

Jeshi la Israel limetoa kanda za video likidai kuonyesha sehemu ya kile walichoelezea kuwa operesheni “nzito” kaskazini mwa Gaza na kusini huko Khan Younis, ikisema imeshambulia miundombinu ya Hamas.

Wapalestina wakiomboleza vifo vya ndugu zao waliouawa katika mashambulizi ya mabomu yanayofanywa na Israeli huko Ukanda wa Gaza nje ya jumba la kuhifadhia maiti huko Khan Younis Dec. 24, 2023.

Wakati huo huo, Wapalestina huko Khan Younis walikusanya miili ya wapendwa wao waliokufa kabla ya mazishi kufuatia mashambulizi ya usiku mzima. Sehemu kubwa ya dunia kwa wiki mbili imekuwa ikitaka kuongezwa kwa muda wa sitisho katika mapigano hayo ili kusambaza misaada inayohitajka sana kwa raia wanaoishi katika maeneo ya wapalestina.

Rais wa Marekani, Joe Biden, amewatakia waandishi wa habari Krismas Njema, na kusema alikuwa na mazungumzo marefu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Biden alielezea kuwa ni mazungumzo ya faragha lakini alisema hakumueleza kutaka sitisho la mapigano.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Wakati huo huo, mjini Tel Aviv, Netanyahu alizungumza katika kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri. Alithibitisha kuhusu mazungumzo yake na Biden, na kuongeza kwamba Israel ni “taifa huru” likiia zingatia kipindi cha vita ambacho hakitasukumwa na mashinikizo ya nje.”

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Mzozo huko Gaza unatishia kusambaa nje ya Mashariki ya Kati huku maafisa wa Marekani wakionya kuongezeka kwa hisia dhidi ya Marekani kutokana na uungaji mkono wa Washington kwa Israel.

Seneta Lindsey Graham, Mrepublican: “Tunaisaidia Israel kukabiliana na uharibifu wa Hamas na kujitetea wenyewe baada ya Oktoba saba. Makundi ya wanajidahi kote duniani yanataka wanachama wao kuishambulia Marekani kama kulipiza kisasi kwa kuisaidia Israel.”

Wizara ya Afya Gaza

Wizara ya Afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas imesema takriban Wapalestina 20,000 wamefariki tangu kampeni dhidi ya kundi hilo ilioazna kufuatia mashambulizi ya Oktoba 7 ambayo yameuwa watu 1,200 nchini Israel. Maafisa wa Marekani wanasema kuna wasi wasi kuwa uungaji mkono wa nchi kwa Israel huenda ukaiweka Marekani katika hali ya wasi wasi.

Wapalestina wakipakia miili ya ndugu zao waliouawa ndani ya Lori katika shambulizi la mabomu lililofanywa na Israeli huko Ukanda wa Gaza watakao zikwa katika makaburi huko Deir al Balah, Ukanda wa Gaza, Dec. 25, 2023.

Lisa Monaco, Naibu Mwanasheria Mkuu: “Mzozo wa sasa unasababisha, nadhani unchangia, na kuongeza mazingira ya tishio. Tunachokiona ni taasisi za kigaidi za kigeni zikichukuoai fursa na kutaka wale wanaowatii kuchukua hatua kufanya kitu fulani. Halafu tunaona watu binafsi na makundi madogo madogo ambayo yanatutia wasi wasi kimsingi yakichukua mwelekeo mwingine katika mzozo huu huko nje ya nchi, na kutokana na picha mbaya tunazoziona ambazo zimekuja kutoka katika ukatili mbaya, mashambulizi mabaya ya kigaidi ambayo yametokea Oktoba saba.”

Sherehe za Krismas Bethlehem

Wakati huu Wakristo wakisherehekea Krismas, usiku mwingine wenye ukimya unajitokeza katika moja ya miji muhimu sana.

Rula Maayah, Waziri wa Utalii wa Palestina: “Dunia yote inasherehekea Krismas mwaka huu lakini siyo Bethlehem. Siyo sehemu aliyozaliwa Yesu Kristo. Bethelehem inasherehekea Krismas kukiwa na majonzi na masikitiko kwa sababu ya kile ambacho kinatokea huko Gaza na kote huko Ukingo wa Magharibi; maeneo yote ya Wapalestina.”

Waombolezaji wakiwa pembeni ya miili ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi ya angani ya Israeli, wakiwa katika hospitali mmoja huko katikati ya Ukanda wa Gaza Disemba 25, 2023. REUTERS/Doaa Ruqaa

Makanisa huko Bethlehem mwaka huu yamepamba na ujumbe wa Nativity wakielezea kuzaliwa kwa Yesu Kristo akiwa kwenye waya na kifusi, kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza. Maafisa hapa wanasema utalii mwaka huu umeshika kutoka milioni 2.3 mpaka Septemba, hakuna hata “mtalii mmoja,” tangu wakati huo.

Ripoti ya Mwandishi wa VOA Arasha Arabasadi.