Wakati ya operesheni huko Gaza, majeshi ya Israel yaliipata miili ya watu wawili walikuwa wamechukuliwa mateka wakati Hamas walipoivamia Israel mwezi Oktoba, kitendo ambacho kililifanya jeshi la Israel kujibu.
Msemaji wa jeshi la ulinzi la Israel alisema Hamas ilikuwa ikiwashikilia mateka chini ya ardhi katika maeneo yenye msongamano mkubwa huko Gaza, na kufanya jitihada za uokoaji kuwa ngumu, lakini amesema Israel haitatetereka katika azma yake ya kumuachilia huru kila mateka.
Mapigano hayo yanayoendelea yamekuja wakati maonyo mapya yametolewa kuhusu athari za vita kwa raia wa Palestina huko Gaza.
“Hatahivyo, janga kubwa, tunalotegemea kuliona ni vifo zaidi vya raia na mateso, , na kuongezeka kwa ukosefu wa makazi ambako kunalitishia eneo hilo,” mkuu wa wakimbizi wa U.N, Filippo Grandi alisema Jumatano.
Papa Francis kwa mara nyingine tena maetoa wito wa kutaka sitisho la haraka la mapigano, wakati akitaka usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwenda Gaza na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.
Ikiwa ni dalili kuwa Marekani inazidi kuwa na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa kiwango cha vifo vya raia kutokana na kampeni ya jeshi la Israel huko Gaza, Rais Joe Biden alimkemea hadharani waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumanne, pamoja na kuwa bado anaiunga mkono kwa dhati Israel.
Forum