Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 23:31

Vituo vya kupiga kura Misri vimefungwa na matokeo yatatangazwa Jumatatu


Mmoja wa raia wa Misri akitumia haki yake ya kupiga kura
Mmoja wa raia wa Misri akitumia haki yake ya kupiga kura

Gazeti la serikali la Al-Ahram liliripoti kuwa Mamlaka ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ina jukumu la kuandaa uchaguzi huo, ilirekodi idadi ya watu waliojitokeza isiyo ya kawaida.

Vituo vya kupiga kura vilifungwa Jumanne nchini Misri baada ya uchaguzi wa siku tatu unaotarajiwa kwa kiasi kikubwa kumrejesha rais aliyeko madarakani Abdel Fattah al-Sisi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu katika ulimwengu wa Kiarabu.

Gazeti la serikali la Al-Ahram liliripoti kuwa Mamlaka ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ina jukumu la kuandaa uchaguzi huo, ilirekodi idadi ya watu waliojitokeza isiyo ya kawaida. Vituo vya kupigia kura vilifunga milango yao saa tatu usiku kwa saa za huko, na matokeo yatatangazwa Jumatatu.

Al-Sisi anatarajiwa kushinda kwa kishindo, licha ya Misri kukumbwa na migogoro mbalimbali ikiwemo vita vya Israel na Hamas katika eneo jirani la Gaza, na mgogoro mbaya zaidi kuwahi kutokea wa kiuchumi nchini humo.

Mkuu huyo wa zamani wa jeshi anagombea kiti hicho dhidi ya ndugu watatu wasiojulikana; Farid Zahran, kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Social Democratic Party; Abdel-Sanad Yamama, kutoka Wafd, chama cha siku nyingi sana lakini kina msimamo wa wastani; Hazem Omar, kutoka chama cha Republican People's Party.

Forum

XS
SM
MD
LG