Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadhi ya wapiga kura hawajaonyesha ari ya kushiriki zoezi hilo, ingawa mamlaka pamoja na wachambuzi kwenye taifa hilo lenye udhibiti mkubwa kwa vyombo vya habari vya ndani, wamekuwa wakiwasihi kushiriki zoezi hilo kwa misingi ya wajibu wa kitaifa.
Makundi ya wapiga kura, baadhi wakiwasili kwa mabasi yameshuhudiwa kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura, vilivyokuwa vikicheza miziki ya kizalendo, ingawa baadhi ya vituo vilikuwa na wapiga kura wachache tu kama ilivyoshuihudiwa na Reuters.
Wakosoaji wamelalamikia zoezi hilo kufuatia muongo mmoja wa misako dhidi ya wapinzani, wakati chombo cha habari cha serikali kikisema ni hatua kuelekea kwenye siasa za vyama vingi.
Forum