Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa uratibu wa masuala ya kibinadamu, UNOCHA, imesema kwamba upelekaji wa misaada umesitishwa kwenye sehemu nyingi za Gaza, isipokuwa huko Rafah karibu na mpaka wa Misri, wakati mapigano makali pamoja na kufungwa kwa barabara muhimu vikizuia operesheni za kibinadamu.
Mapigano hayo yanakadiriwa kuwakoseshwa makazi takriban watu milioni 1.9 kutoka Gaza, wengi wao wakitafuta hifadhi upande wa kusini, ambako kuna msongamano mkubwa sana, huku maonyo yakitolewa kwa hali mbaya ya usafi wa vyoo, na tishio la kuongezeka kwa magonjwa kuambukiza.
UNOCHA imesema kwamba maelfu ya watu wamewasili Rafah katika kipindi cha wiki moja iliyopita. Katika kipindi hicho, Israel imeongeza mashambulizi yake dhidi ya wanamgambo wa Hamas upande wa kusini, ikiwemo operesheni zake katika mji wa Khan Younis ambao ni wa pili kwa ukubwa huko Gaza.
Forum