Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 23:22

Duru ya kwanza ya upigaji kura uchaguzi mkuu Misri 2024 yakamilika leo


Wamisri wakisubiri kupiga kura huko Arish, Misri, Dec. 10, 2023. (Hamada Elrasam/VOA)
Wamisri wakisubiri kupiga kura huko Arish, Misri, Dec. 10, 2023. (Hamada Elrasam/VOA)

Jedwali la shughuli za upigaji kura kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Misri linaonyesha siku ya Jumanne tarehe 12 ndio hitimisho kwa duru ya kwanza katika mchakato wa kumchagua rais kupitia kura za raia milioni 67 wenye sifa za kushiriki kuanzia umri wa miaka 18.

Zoezi hili la siku tatu lilianza tarehe 10 ambapo wapiga kura katika mikoa 27 walielekea kwenye vituo vya kupigia kura vilivyofunguliwa tangu saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku, wengi wao wakiwa na matarajio makubwa ya kwamba rais aliyopo madarakani anatazamiwa kushinda tena awamu nyingine ya tatu.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kwamba matokeo ya kura zilizopigwa yatatangazwa tarehe 18 mwezi huu na kisha wapiga kura kungojea mzunguko mwingine wa pili wa upigaji kura katika kipindi cha mwezi Januari 2024.

Wakati huo huo nchi inaendelea kupitia hali ngumu ya kiuchumi ambapo pia kuna changamoto ya vita katika mipaka yake na Ukanda wa Gaza.

Wagombea wa Kiti cha Urais 2024.

Waliopitishwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa kuwania kiti cha urais baada ya rais aliyeko madarakani Abdel Fattah Elsisi ni Farid Zahran kupitia ‘chama cha Kidemokrasia cha Jamii ya Wamisri’, mwingine ni Abdel-sanad Yamama kupitia ‘Chama cha El Wafd’ na Hazem Omar kupitia ‘Chama cha Republican’.

Kwa mujibu wa tume hiyo shughuli za upigaji kura katika mikoa yote kupitia vituo vyake vikuu 9376 na matawi ya idara zake 11631 zinafanyika chini ya usimamizi na ungalizi kutoka pande mbali mbali, zikiwemo taasisi za kiraia za ndani na za kimataifa, ikijumuisha majaji elfu 15 kufuatilia mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Zaidi ya hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari Mwanasheria Ahmed Bendari, mkurugenzi wa kamati ya utendaji kwenye bodi ya tume hiyo akifafanua na kuonyesha uaminifu wa usimamizi wao kwenye shughuli za uchaguzi amesema: “kwa hakika tume ya uchaguzi ni huru imekamilika na ipo chini ya katiba na sheria na mamlaka yake kwa ajili ya kuweka kanuni zinazoendena na shughuli za uchaguzi wa urais….”

Ushiriki wa raia katika upigaji kura

Mpaka inafikia leo ikiwa ni siku ya tatu na ya mwisho katika duru ya kwanza ya shughuli za uchaguzi mkuu nchini Misri, hali za kiusalama na mwitikio wa wapiga kura zimeendelea kushuhudiwa kuwa ni tulivu katika maeneneo mbali mbali yaliyotengwa kwa ajili ya wapiga kura, ikijumuisha shule, na kumbi za vijana pamoja na maeneo ya wazi ya vituo vya afya.

Upigaji kura ndani ya taifa la Misri ulitanguliwa na upigaji kura mwingine siku chache zilizopita nje ya taifa kwa raia wake wanaoishi ughaibuni au waliopo safarini kwa muda ndani ya kipindi cha uchaguzi, ambapo kupitia balozi 137 na jumbe za kidiplomasia 121 raia hao walitumia siku tatu kuanzia tarehe 1,2 na 3 mwezi Desemba ili kushiriki kupiga kura.

Forum

XS
SM
MD
LG