Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:57

Misri yaendelea kupinga kuondoshwa wapalestina katika ardhi yao.


Viongozi wa serekali ya Misri wakijadili kuhamishwa kwa Wapalestina huko Ukanda wa Gaza
Viongozi wa serekali ya Misri wakijadili kuhamishwa kwa Wapalestina huko Ukanda wa Gaza

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry amesema kwamba mawasiliano katika Hamas na Misri bado yanaendelea, na serikali yake inaendeleza juhudi hizo pia na washirika wengine kimataifa ili kuwaachilia huru mateka waliopo Ukanda wa Gaza.

Alhamisi jioni akiwa kwenye kikako maalum na waandishi wa habari wanaoripotia mashirika ya habari ya kigeni, Waziri Shoukry akijibu swali linaloangazia uvumi wa kuwa Israel na Marekani zinaishinikiza nchi yake kukubali suala la kuhamishwa raia wa Palestina waliopo huko ukanda wa Gaza ili Misri ifutiwe madeni.

Shoukry amekanusha kuwepo kwa jambo hilo na ni taarifa zisizo sahihi, akiongezea kuwa haiwezekani kuaondoa raia hao nje ya ardhi yao, akitilia mkazo juu ya kadhfa hii Waziri Shoukry amesema: “Tunatumai kuwa juhudi zetu zitapelekea kuachiliwa kwa haraka mateka”

Katika taarifa za awali Israel ililiripoti kuwa Wapiganaji wa Hamas waliwakamata raia wake 240 wakati wa shambulio la kushtukiza kwenye maeneo ya walowezi yanayoizunguka Gaza tarehe 7 mwezi Oktoba.

Mapigano ukanda wa Gaza

Hadi kufikia siku ya Alhamisi mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yameshafikia siku 41, wanajeshi wa Israel wameendelea kuishambulia Gsza huo wakiwasaka na kukabiliana na wapiganaji wa Hamas huku wakisababisha vifo vya raia wasio na hatia ambapo idadi yake ni zaidi ya 11,000 kufuatia athari za mabomu ya moja kwa moja hali ambayo inatajwa kuwa ni ukikukwaji wa kanuni za kimataifa na uvunjaji wa haki za raia wa Palestina.

Maafisa wa Misri wakiwa katika mkutano kuhusu Gaza, Palestina
Maafisa wa Misri wakiwa katika mkutano kuhusu Gaza, Palestina

Kwa mujibu wa afisa wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa ni kwamba kuna juhudi zinafanyika ili kuihamisha hospitali ya Al Shifaa ambayo imevamiwa na wanajeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza lakini bado vikwazo vya kiusalama vinakwamisha juhudi hizo.

Rick Brennan mkurugenzi katika idara ya dharura ya WHO kwenye ukanda huo ameongeza kusema kuwa shirika la msaada la Hilali Nyekundu ndani ya Palestina nalo pia halina mafuta ya kuendesha gari za wagonjwa kutoka sehemu moja hadi nyingine ndani ya Gaza, na ama kwa upande wa Misri magari yapo ya kuwahamisha wagonjwa licha pia bado kunakosekana dhamana ya usalama njiani.

Forum

XS
SM
MD
LG