Katika nchi ambayo imekumbwa na msukosuko mkubwa wa kifedha katika historia yake ya hivi karibuni mfumuko wa bei umekaribia asilimia 40 baada ya sarafu ya nchi kupoteza nusu ya thamani yake na kupanda kwa gharama za uagizaji bidhaa na kufanya uchumi kuwa ajenda muhimu kwa raia wa Misri.
Hata kabla ya mzozo wa sasa, karibu theluthi mbili ya watu takriban milioni 106 nchini humo walikuwa wakiishi katika umaskini.
Kabla ya vituo vya wapiga kura kufunguliwa mamia ya wapiga kura walifurika katika vituo jijini Cairo, huku kukiwa na ulinzi mkali ameripoti mwanahabari wa AFP.
Upigaji kura utafanyika kuanzia Jumapili hadi Jumanne, kati ya saa tatu asubuhi mpaka saa tatu usiku na matokeo yatatangazwa Desemba 18.
Forum