Jeshi la Israel limesema kwamba linatadhmini ripoti za shambulizi hilo huko Maghazi, wakati likisisitiza nia yake ya dhati ya kupunguza madhara kwa raia katika vita dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas.
Israel pia imeripoti vifo zaidi miongoni mwa wanajeshi wake kuanzia Ijumaa kuwa 17, wakati jumla ya vifo tangu kuanzisha operesheni ya ardhini huko Gaza ikifikia 156. Mashambulizi ya Israel ambayo yamehusisha maelfu ya mashambulizi ya anga pamoja na operesheni za ardhini yameacha sehemu kubwa za Gaza zikiwa imeharibiwa, pamoja na vifo vya takriban wapalestina 20,400, kulingana na wizara ya afya ya Gaza.
Mapigano hayo pia yamewakosesha makazi wakazi wengi wa Gaza takriban milioni 2.3, huku wengi wao wakitafuta hifadhi kwenye maeneo ya Umoja wa Mataifa yenye msongamano mkubwa kusini mwa Gaza.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili ameapa kuendelea na kile amekisema ni 'vita vya muda mrefu, hadi pale vikosi vya Israel vitakapo waangamiza Hamas na kurejesha usalama.'
Forum