Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:42

Israel yasema imekaribia kuchukua udhibiti kamili wa kaskazini mwa Gaza


Majengo yalioharibiwa na mashambulizi ya Israel kwenye mji wa Jabalia, Ukanda wa Gaza hapo Oct. 11, 2023.
Majengo yalioharibiwa na mashambulizi ya Israel kwenye mji wa Jabalia, Ukanda wa Gaza hapo Oct. 11, 2023.

Jabalia ambao ni mji uliopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza umelengwa usiku kucha katika mashambulizi ya Israel pamoja na mapigano ya Jumapili asubuhi, wakati Israel ikisema kwamba imekaribia kuchukua udhibiti kamili wa kaskazini mwa Gaza.

Ripoti zimeongeza kwamba Israel imelenga takriban malengo 200 ndani ya Gaza, katika muda wa siku moja iliyopita. Msemaji wa jeshi la Israel Jonathan Conricus ameambia shirika la habari la AFP kwamba, “Sasa tunaelekeza juhudi zetu za mashambulizi dhidi ya Hamas kusini mwa Gaza.”

Hamas imesema kwamba mashambulizi hayo yamegonga Jabalia na Khan Younis ambayo ni miji ya kuzaliwa na pia ngome za Yahya Sinwar, ambaye ni kiongozi wa Hamas huko Gaza. Mjemaji wa jeshi la Israel la IDF, Rear Admiral Daniel Hagari, amesema kwamba vikosi vyake vinakaribia kuchukua udhibiti kamili kaskazini mwa Gaza.

Hata hivyo zaidi ya darzeni moja ya wanajeshi wa Israel walikufa kwenye mapigano ya mwishoni mwa wiki, katika kile Israel imetaja kuwa siku za mapigano mabaya zaidi, tangu ilipoanza mashambulizi ya ardhini ndani ya Gaza hapo Oktoba 20. Ripoti za mapema Jumapili kutoka Israel zinasema kwamba wanajeshi wake 153wameuwawa tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7.

Forum

XS
SM
MD
LG