Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 11:14

Israel inasema itachukua miezi kadhaa kuwashinda wanamgambo wa Hamas


Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant akizungumza katika kituo cha jeshi cha Kirya. Israel, Oct. 28, 2023.
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant akizungumza katika kituo cha jeshi cha Kirya. Israel, Oct. 28, 2023.

Hamas imekuwa ikijenga miundombinu yake chini ya ardhi na juu ya ardhi huko Gaza, kwa zaidi ya muongo mmoja na kwamba kuliangamiza kundi hilo la Ki-islamu kutahitaji muda mrefu. Itachukua zaidi ya miezi kadhaa. Lakini tutashinda, na tutawaangamiza, alisema Gallant.

Mkuu wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amemwambia mshauri wa usalama wa taifa wa White House, Jake Sullivan siku ya Alhamisi kwamba itachukua miezi kadhaa kwa vikosi vya Israel kuwashinda wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Amesema Hamas imekuwa ikijenga miundombinu yake chini ya ardhi na juu ya ardhi huko Gaza, kwa zaidi ya muongo mmoja na kwamba kuliangamiza kundi hilo la Ki-islamu kutahitaji muda mrefu. Itachukua zaidi ya miezi kadhaa. Lakini tutashinda, na tutawaangamiza, alisema Gallant.

Hakukuwa na maoni ya haraka ya Marekani juu ya mazungumzo ya Sullivan na Gallant. Huku vita vya Israel na Hamas huko Gaza vikiingia mwezi wa tatu, ofisi ya Gallant imesema maafisa hao wawili pia walijadili umuhimu wa kuwarejesha Wa-israeli katika nyumba zao karibu na mpaka na Lebanon kuelekea kaskazini, baada ya maelfu ya watu waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran.

Forum

XS
SM
MD
LG