Israel inaomboleza vifo vya mateka watatu wa Israel waliouawa kimakosa na wanajeshi wa Israel wakati wa operesheni yake ya ardhini katika Ukanda wa Gaza.
Msemaji mkuu wa jeshi hilo, Admirali Daniel Hagari, amesema vikosi vya Israel viliwatambua kimakosa mateka hao kama tishio, na kuwafyatulia risasi Ijumaa. Alisema kuwa haijafahamika iwapo mateka hao waliwatoroka watekaji wao, au walikuwa wametelekezwa.
Vifo vyao vilitokea katika eneo la Shijaiyah huko Gaza City, eneo la mapigano ya umwagaji damu kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hamas. Alisema jeshi limeelezea masikitiko makubwa na linafanya uchunguzi.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameyataja mauaji ya mateka hao kuwa ni “janga lisilovumilika” na kuahidi kuendelea “kwa juhudi kubwa za kuwarejesha mateka wote nyumbani wakiwa salama”.
Forum