Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:51

Jeshi la Israel linasema wanajeshi wake 10 waliuawa Ukanda wa Gaza

Wanajeshi wa Israeli wakiwa karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza huko kusini mwa Israel. Dec. 11, 2023.
Wanajeshi wa Israeli wakiwa karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza huko kusini mwa Israel. Dec. 11, 2023.

Jeshi la Israel limesema limeshambulia zaidi ya maeneo 250 yaliyolengwa katika siku za hivi karibuni. Mashambulizi ya anga ya Israel ni pamoja na kushambulia kile jeshi lilisema ni timu ya Hamas inayojiandaa kurusha roketi nchini Israel.

Jeshi la Israel limesema Jumatano kuwa wanajeshi wake 10 waliuawa katika mapigano huko Ukanda wa Gaza katika kampeni yake ya kuwaondoa wanamgambo wa Hamas kutoka eneo la Palestina, huku Rais Joe Biden akikutana na familia za mateka wa Marekani wanaoshikiliwa na kundi hilo jumatano.

Jeshi la Israel limesema limeshambulia zaidi ya maeneo 250 yaliyolengwa katika siku za hivi karibuni. Mashambulizi ya anga ya Israel ni pamoja na kushambulia kile jeshi lilisema ni timu ya Hamas inayojiandaa kurusha roketi nchini Israel.

Wakati wa operesheni huko Gaza, vikosi vya Israeli vilipata miili ya watu wawili waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Hamas mwezi Oktoba ambalo lilichochea Israel kujibu kwa njia ya jeshi.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema Hamas inawashikilia mateka katika maeneo ya chini ya ardhi yaliyojaa watu wengi huko Gaza, na kufanya juhudi za uokozi kuwa ngumu lakini amesema Israel haitazuiwa katika operesheni yake ya kuhakikisha kila mateka anakuwa huru.

Forum

XS
SM
MD
LG