Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:47

Malori zaidi ya misaada yaingia kusini mwa Gaza kupitia mpaka wa Rafah


Malori yaliobeba misaada ya kibinadamu yakiingia Gaza kwenye mpaka wa Misri wa Rafah.
Malori yaliobeba misaada ya kibinadamu yakiingia Gaza kwenye mpaka wa Misri wa Rafah.

Ripoti za mapema Jumamosi zinasema kwamba malori 70 ya misaada ya kibinadamu yameingia kusini mwa Gaza kupitia kwenye mpaka wa Misri wa Rafah.

Gaza inahitaji pakubwa misaada ya kibinadamu, na Israel ilikuwa imeomba wakazi wa Gaza kuelekea upande salama kusini mwa Gaza, lakini wengi walikosa makazi baada ya kufika, kutokana na msongamano mkubwa wa watu. Wakati huo huo baada ya siku kadhaa za mazungumzo kuhusu sitisho la muda la mapigano kwa misingi ya kibinadamu, pamoja na upelekaji wa misaada kwenye Ukanda wa Gaza, Marekani Ijumaa ilisusia pendekezo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lenye wanachama 15, la kuruhusu hatua hiyo.

Balozi wa Marekani kwenye UN Linda Thomas-Greenfield amesema kwamba ni lazima mateka wanaoshikiliwa waachiliwe mara moja, na kwamba wote Israel na Hamas ni lazima waheshimu sheria za kimataifa. Ameongeza kusema kwamba Marekani hajaridhishwa na pendekezo lililotolewa na Baraza hilo, kwa kuwa halijakemea shambulizi la Hamas la Oktoba 7 lililoua watu 1,200 ndani ya Israel. Russia ambayo ilitaka Israel ikemewe kwenye pendekezo hilo, pia ilisusia kupiga kura, ikitaja rasimu ya mwisho iliyokuwa na marekebisho yaliopendekezwa na Washington kuwa ‘isiyo na ushawishi wala uwezo wowote.’

Forum

XS
SM
MD
LG