Mtiririko wa yaliyotokea kipindi cha kumfungulia mashtaka Rais Trump
Kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell akielekea katika ukumbi wa Seneti wa Bunge la Marekani Capitol Hill Washington, Alhamisi, Disemba. 19, 2019. (AP Photo/Susan Walsh)
Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi akizungumza kabla ya vifungu viwili vya kumfungulia mashtaka Rais Donald Trump kupigiwa kura katika Baraza la Wawakilishi, katika jengo la bunge la Capitol Hill Washington, Disemba 18, 2019.
Spika Nancy Pelosi akitabasamu wakati Baraza la Wawakilishi likiendelea kupiga kura kupitisha vifungu viwili vya kumfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Donald Trump Washington, Dec. 18, 2019.
Kura za Wawakilishi zikionyeshwa katika Runinga wakati wa kupiga kura iliyokuwa inasimamiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi.
Kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell, akiwa na Sen. Roy Blunt, Kushoto na Sen. Joni Ernst, kulia, akipinga mchakato wa kumfungulia mashtaka Rais Donald Trump (AP Photo/J. Scott Applewhite)
Rais Donald Trump akizungumza na wabunge wa chama cha Republik siku moja baada ya Baraza la Wawakilishi kupitisha vifungu vya kumfungulia mashtaka kumuondoa madarakani.
Kura zilizopigwa katika Baraza la Wawakilishi zikionyeshwa katika runinga.
Mtu akiandamana nje ya bunge la Marekani Washington, DC Disemba 18, 2019 wakati baraza la Wawakilishi likijadili vifungu viwili vya kumfungulia mashtaka Rais Donald Trump. (Photo by Alex Edelman / AFP)
Viongozi wa Bunge la Marekani Alhamisi wakijadili hatua zinazofuata katika Baraza la Seneti wakati tayari Baraza la Wawakilishi limemfungulia mashtaka Rais Donald Trump.