Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:22

White House inaelekea kukubali upo uwezekano wa Trump kushtakiwa


Rais Donald Trump (Kushoto), Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi
Rais Donald Trump (Kushoto), Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi

White House baada ya kupinga kwa miezi kadhaa suala la uchunguzi wa Baraza la Wawakilishi kumshtaki kumuondoa rais madarakani, sasa inaelekea kukubali kwamba kuna uwezekano wa suala hilo kufika kwenye Baraza la Seneti linalodhibitiwa na warepublikan. 

Rais Donald Trump aliwashinikiza Wademokrat katika ujumbe wa tweet Alhamisi, "iwapo mnataka kunifungulia mashtaka kuniondoa madarakani, fanyeni hivi sasa, kwa haraka ili kuwepo uadilifu... katika kesi katika Baraza la Seneti, na ili nchi irejee katika shughuli zake," Rais Donald Trump alisema.

Ni ujumbe alioutoa hata kabla ya Spika wa Baraza la wawakilishi Nancy Pelosi kuwaambia viongozi wa chama cha democrat siku ya alhamisi kuendelea na hatua ya kutaka kufungua mashitaka dhidi ya rais akitangaza rasmi kwamba Trump ametumia vibaya madaraka yake.

Pelosi, katika tamko fupi lenye machachari, alipinga kuwa kiongozi wa Republikan alikinzana na desturi za mwenendo wa urais, akikiuka kiapo alichochukuwa kuilinda Katiba ya Marekani kwa kuitaka Ukraine ianzishe uchunguzi wa hasimu wake mkuu wa Chama cha Demokratik atakaye chuana naye 2020, Makamu wa Rais Joe Biden, ili iweze kuwa ni msaada kwake wakati atakapogombea tena nafasi ya urais.

“Ukweli haupingiki,” Pelosi amesema. “Rais ametumia mamlaka yake vibaya kwa maslahi binafsi ya kisiasa kwa gharama ya usalama wa taifa letu."

Pelosi alimtaka Mwakilishi Jerrold Nadler, mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Baraza la Wawakilishi ambapo uchunguzi wa kumfungulia mashtaka na kumuondoa madarakani rais umeanza Jumatano, na wanakamati wengine wa chama cha Demokratik kuandaa rasimu ya vifungu vya kumfungulia mashtaka.

Wakati Pelosi hajataja tarehe zozote za kufunguliwa mashtaka, Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Wademokrat wanaweza kupiga kura ya kumfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani Trump kabla ya mapumziko ya sikukuu ya Krismas mwisho wa mwezi wa Disemba.

Hiyo itatoa fursa kwa kesi kuanza mwezi Januari katika Baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublikan, ambapo kukutikana na hatia kwa Trump na kuondolewa madarakani kunaonekana siyo jambo linalotarajiwa.

XS
SM
MD
LG