Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:31

Mashtaka dhidi ya Rais Trump yaanza kujadiliwa Baraza la Wawakilishi


Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump

Rais Donald Trump anakabiliwa na mchakato ambao unaweza kumalizika na uamuzi wa kumuondoa katika wadhifa wake wa urais wa Marekani.

Hivi sasa Baraza la Wawakilishi linakuwa kama jopo la ushauri la mahakama ambalo litaangalia kwa undani iwapo Rais Trump anamakosa ya kujibu.

Hata hivyo mchakato huu ni wa kisiasa siyo mchakato wa kesi ya jinai.

Mahojiano yanayoanza Jumapili katika Baraza la Wawakilishi ni sehemu ya awali ya kile kilichoainishwa katika Katiba ya Marekani.

Katika hatua hii ya kufunguliwa kesi Baraza la Wawakilishi linajukumu la kukusanya ushahidi ambao watautumia kufungua kesi dhidi ya Rais Donald Trump.

Matokeo ya utaratibu huo yatapelekea hatua ya baraza zima la wawakilishi kupiga kura ya kumfungulia mashitaka ya kumwondoa rais madarakani ama la.

Iwapo atafunguliwa mashtaka kesi itasikilizwa katika Baraza la Seneti, ikiendeshwa na Jaji Mkuu.

Baraza la Wawakilishi la Marekani tayari lilikwisha pitisha azimio la kuruhusu rasmi uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump na umekamilika.

Azimio hilo liliwezesha baraza hilo kufanya mahojiano katika vikao na watu mbalimbali ambavyo vitaweza kuonekana na kusikika mubashara na wananchi kupitia vyombo vya habari.

Mashahidi tayari waliitwa mbele ya kamati ya baraza hilo kutoa maelezo juu ya madai mbalimbali yaliyotolewa dhidi ya Rais Trump.

Hata hivyo Rais amesisitiza kuwa hajafanya makosa yoyote wakati alipozungumza na kiongozi huyo.

Bunge pamoja na mambo mengine imechunguza iwapo kulikuwa na masharti yoyote ambayo Rais aliipa Ukraine, iwapo wanataka msaada wa Marekani uwafikie.

Hatua hiyo ilifungua hatua nyingine mpya ya kufanya vikao vya wazi ambapo watu kadha wataitwa mbele ya kamati ya sheria na rais kupata fursa ya kuwa na wakili wa kumtetea mbele ya kamati hiyo. Wajumbe warepublican katika kamati hiyo pia nao watapata fursa ya kuita mashahidi wao wenyewe.

XS
SM
MD
LG