Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:34

Baraza la Wawakilishi : Mahojiano ya hadhara yakimlenga Trump kuanza wiki ijayo


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Mahojiano ya hadhara yakumchunguza Rais Donald Trump na juhudi zake za kuishinikiza Ukraine kumchunguza mmoja wa wapinzani wake wa chama cha Demokrat aliyekabiliana naye katika uchaguzi wa mwaka 2020 yataanza wiki ijayo, mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Baraza la Wawakilishi Adam Schiff amesema Jumatano.

Baada ya wiki kadhaa za mahojiano yaliyofanyika faragha, Schiff amesema Wamarekani watapata nafasi ya “kuyapima madai hayo” dhidi ya Trump.

“Sehemu kubwa ya ushahidi haupingiki,” amesema Schiff.

Amepinga kuwa madai ya msingi yanayo mkabili Trump “anapojaribu kuifanya Ukraine ichunguze makosa ya hasimu wa kisiasa,” aliyekuwa Makamu wa Rais Joe Biden, mmoja wa viongozi kati ya kundi la Wademokrat wanaojaribu kushinda uteuzi wa nafasi ya urais wa chama chao ili waweze kukabiliana na Trump uchaguzi wa mwaka 2020.

Schiff alisema jopo la kamati ya usalama litasikiliza maelezo kutoka kwa Bill Taylor, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani nchini Ukraine, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje George Kent wakati mahojiano hayo yatakapofanyika Jumatano ijayo.

Wawikilishi wa Chama cha Republikan wamekosoa jinsi Wademokrat waliowengi wanavyoendesha uchunguzi wa kumuondoa Trump madarakani, wakisema mchakato huo umekuwa wa siri na kuwa Warepublikan hawapewi fursa sawa kushiriki katika mchakato huo.

Lakini Wademokrat wanasema Wawakilishi wa chama cha Republikan na wasaidizi wao wamepewa nafasi sawa kuwahoji mashahidi.

XS
SM
MD
LG