Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:25

Suala la uchunguzi wa Trump latawala katika mdahalo wa Wademokrat

Walioshiriki Mdahalo : Wagombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokrat Senata Cory Booker, Mwakilishi Tulsi Gabbard, Seneta Amy Klobuchar, Meya wa South Pete Buttigieg, Seneta Elizabeth Warren, aliyekuwa Makamu wa Rais Joe Biden, Seneta Bernie Sanders na Senator Kamala Harri

Suala la uchunguzi wenye azma ya kumshtaki ili kumuondoa madarakani Rais Donald Trump lilitawala wakati wa mdahalo mjini Atlanta Jumatano usiku.

Wengi wa Wademokrat wanaowania kupata uteuzi wa kugombea urais wa Marekani, walionekana kukubaliana na hatua hiyo.

Seneta Bernie Sanders alimtaja Trump kuwa rais fisadi zaidi katika historia ya Marekani huku akitahadharisha wenzake kuzingatia mambo mengine mbali ya kumpinga Trump katika juhudi ya kumshinda kwenye uchaguzi ujao.

Sanders aliangazia changamoto za wale wasiokuwa na bima ya afya, ukosefu wa makazi bora, pamoja na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.

Seneta Elizabeth Warren alisema kuwa suala la bunge kutomchukulia hatua Trump hata baada ya ripoti ya Muller kutolewa ikiihusisha Russia kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani 2016, limempa nguvu Trump.

Seneta huyo amedai kuwa hilo limepelekea kujihusisha kwenye kashfa ya sasa ambapo anakabiliwa na shutuma kuwa aliishinikiza Ukraine kumchunguza hasimu wake wa kisiasa wa zamani Joe Biden huku akizuia misaada ya kijeshi kwa Kyiv.

XS
SM
MD
LG