Bw. Schiff alisema Jumanne kuwa huwenda wakaendelea na utaratibu wa kumfungulia mashtaka Rais Trump, baada ya wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani kumuamrisha balozi wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Ulaya Gordon Sondland, kutokufika mbele ya ya kamati 3 za baraza za wawakilishi, ili kujieleza kuhusu jukumu lake katika mawasiliano ya simu yenye utata kati ya Rais Trump na viongozi wa Ukraine.
Trump ametetea amri hio kwenye ujumbe wa Twitter akiandika kwamba Sondland angelikuwa anatoa ushahidi mbele ya mahakama iliyo na upendeleo na ambayo haki za Warepublican zimeondolewa na ukweli wa mambo hauruhusiwi kutangazwa ili wananchi waweze kuona.
Kamati 3 za baraza la bunge zilikuwa zimepanga kumhoji Balozi Sondland mapema Jumanne. Sondland amekuwa katika siku za karibuni mashuhuri kwa kutajwa kwake kwenye uchunguzi unaoendelea, kutokana na juhudi zake za kuitaka Ukraine kumchunguza mtoto wa mpinzani mkuu wa Rais Trump katika kinyanganyiro cha urais kwenye uchaguzi ujao wa 2020 Joe Biden.