Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:43

Uturuki yapinga hatua ya Russia kukalia kwa mabavu ardhi ya Ukraine


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema Jumamosi kuwa inapinga ukaliaji kimabavu wa Russia katika mikoa minne ya Ukraine, na kuongezea kuwa uamuzi huo “ni ukiukaji mkubwa” wa sheria za kimataifa.

Uturuki, mwanachama wa NATO, imekuwa ikifanya kitendo cha kuleta upatanishi tangu Russia ilipoivamia Ukraine Februari 24. Ankara inapinga vikwazo vya Magharibi kwa Russia na ina uhusiano wa karibu na Moscow na Kyiv, jirani zake wa Black Sea. Pia imekosoa uvamizi wa Russia na kupeleka ndege zisizotumia rubani ‘drone’ kwa Ukraine.

Wizara ya Uturuki ilisema Jumamosi kuwa haijtambua uingiliaji kati wa Russia huko Crimea mwaka 2014, na kuongezea kwamba inapinga uamuzi wa Russia kujiingiza katika mikoa minne, Doetsk, Luahnsk, Kherson na Zaporizhzhia.

“Uamuzi huu, ambao unahusisha ukiukaji mkubwa sana wa misingi ya sheria za kimataifa, hauwezi kukubaliwa hata kidogo,” wizara imesema.

“Tunasisitiza uungaji mkono wetu kwa suluhisho kwa vita hivi, ambavyo ukali wake unaendelea kukua, kwa kuzingatia amani ya haki itakayopatikana kupitia mazungumzo,” taarifa iliongezea.

Rais wa Russia Vladimir Putin akihutubia mkutano wa maadhimisho ya majeshi yake kuingia kwa mabavu katika mikoa minne ya Ukraine iliyovamiwa na majeshi ya Russia, huko Moscow Sept. 30, 2022. Maneno juu ya picha yake yanamaanisha "Milele Tukopamoja."
Rais wa Russia Vladimir Putin akihutubia mkutano wa maadhimisho ya majeshi yake kuingia kwa mabavu katika mikoa minne ya Ukraine iliyovamiwa na majeshi ya Russia, huko Moscow Sept. 30, 2022. Maneno juu ya picha yake yanamaanisha "Milele Tukopamoja."

Rais wa Russia Vladimir Putin alitangaza Ijumaa kujiingiza katika mikoa minne, akiahidi Moscow itahsinda katika “operesheni zake maalum za kijeshi” hata wakati ikiklabiliwa na hali mpya isiyo ya kawaida ya kijeshi.

Tangazo lake limekuja baada ya Russia kufanya kile ilichokiita kura ya maoni katika maeneo inayoyakalia kimabavu nchini Ukraine. Serikali za Magharibi na Kyiv ilisema kuwa kura hiyo ilikiuka sheria za kimataifa na ilikuwa kandamizi na isiyokuwa na uwakilishi.

Marekani, Uingereza na Canada zilitangaza vikwazo vipya ikiwa ni majibu yake kwa hatua za Russia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Ijumaa nchi yake imewasilisha ombi la haraka la kujiunga na muungano wa NATO na hatafanya mazungumzo ya amani na Russia wakati Putin bado ni rais.

XS
SM
MD
LG