Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:43

Upigaji kura wafanyika katika maeneo manne  ya Ukraine


Mtazamo wa jumla unaonyesha jiji linalodhibitiwa na Urusi la Kherson, Ukrainia Julai 24, 2022. REUTERS/Alexander Ermochenko/
Mtazamo wa jumla unaonyesha jiji linalodhibitiwa na Urusi la Kherson, Ukrainia Julai 24, 2022. REUTERS/Alexander Ermochenko/

Upigaji kura unatarajiwa kufungwa Jumanne katika uchaguzi ulopangwa na maafisa walowekwa na Rashia katika majimbo manne ya Ukraine inayokalia, serikali ya Ukraine na washirika wake wa magharibi wakipinga uchaguzi huo na kuueleza ni udanganyifu.

Msemaji wa White House Karine Jean-Pierre aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba “Tunasimama na washirika wetu kote duniani katika kupinga matokeo yoyote ya uwongo ambayo Russia itatangaza,”.

Kwa kadiri tunachofanya, tuko tayari kuweka vikwazo vya ziada vikali na haraka vya kiuchumi dhidi ya Russia pamoja na washirika wetu, kujibu vitendo hivi ambavyo tunaona kwa sasa ikiwa vitasonga mbele na kuchukua majimbo hayo” Jean. - Pierre alisema. "Tumekuwa wazi sana juu ya hilo."

Upigaji kura ulianza Ijumaa katika majimbo ya Luhansk na Kherson inayodhibitiwa na Russia, na katika maeneo yanayokaliwa ya majimbo ya Donetsk na Zaporizhzhia. Katika baadhi ya matukio, wanajeshi wa Russia wamekuwa wakienda nyumba kwa nyumba kuwaamuru raia wa Ukraine kwa mtutu wa bunduki kupiga kura.

XS
SM
MD
LG