Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:03

Uingereza yafafanua aina ya makombora yaliyotumiwa na Russia kuushambulia msafara wa kibinadamu


Watu wamekusanyika kusherehekea kuingizwa mikoa ya Ukraine katika himaya ya Russia, huko Sevastopol, Crimea, Sept. 30, 2022. T
Watu wamekusanyika kusherehekea kuingizwa mikoa ya Ukraine katika himaya ya Russia, huko Sevastopol, Crimea, Sept. 30, 2022. T

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi kuwa makombora yaliyotumika kuushambulia msafara wa kibinadamu nchini Ukraine “kuna uwezekano mkubwa likawa ni kombora la ulinzi wa anga la masafa marefu la Russia lililotumika katika shambulizi la ardhini.”

Wizara ilisema katika ripoti ya upelelezi iliyobandikwa katika Twitter kwamba matumizi ya “silaha za hali ya juu” katika shambulizi la ardhini karibu na Zaporizhzhia “bila ya shaka limesukumwa na upungufu wa silaha za kawaida, hususan makombora yenye shabaha ya masafa marefu.”

Ripoti hiyo ilisema shambulizi lililofanyika Ijumaa katika siku ambayo Rais wa Russia Vladimir Putin alitangaza kujiingiza katika mikoa minne ya Ukraine, ikiwemo Zaporizhzhia, ilipelekea kwa Russia “kuua raia ambao hivi sasa inadai ni raia wake.” Takriban watu 23 waliuawa na wengine 28 walijeruhiwa katika shambulizi lililowalenga watu waliokuwa wanatafuta njia ya kuwaokoa ndugu zao kutoka katika eneo lililokuwa linakaliwa kimabavu. Takriban watu watatu waliuawa katika shambulizi jingine huko Mykolaiv, huku watu wasiopungua 12 walijeruhiwa.

“Ni hulka ya kiu cha umwagaji damu!” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliandika katika ujumbe wa Telegram. “Bila shaka utatoa majibu. Kwa kila kifo cha mwananchi wa Ukraine!”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Siku ya Ijumaa, Putin alitangaza kuingia katika mikoa ya Ukraine, hata pale Ukraine ilipotangaza kuwa jeshi lake lilikuwa linapata mafanikio makubwa upande wa mashariki mwa nchi hiyo.

“Watu wanaoishi huko Luhansk, Donetsk, mkoa wa Kherson na mkoa wa Zaporizhzhia wanaendelea kuwa ni mashujaa wetu milele, “Putin alisema katika tafrija siku ya Ijumaa huko Kremlin.

Zelenskyy alijibu katika hotuba yake ya Ijumaa jioni kwa njia ya video akisema, “Tumepata matokeo muhimu upande wa mashariki mwa nchi yetu … kila mtu amesikia kile kinachoendelea huko Lyman.

Hata pale Putin aliposonga mbele na hatua ya kunyakua maeneo ya Ukraine Ijumaa, majeshi ya Ukraine yaliwazunguka mamia ya wanajeshi wa Russia katika moja ya vituo vikuu vya kuhifadhi silaha upande wa kaskazini mwa Donetsk, karibu na mji wa Lyman.

Rais wa Russia Vladimir Putin akiungana na wakuu waliochaguliwa na Moscow kutawala katika maeneo ambayo Russia imeingia kwa mabavu.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiungana na wakuu waliochaguliwa na Moscow kutawala katika maeneo ambayo Russia imeingia kwa mabavu.

Kiongozi aliyewekwa na Russia katika jimbo la Donetsk nchini Ukraine, Denis Pushilin, alikiri kuwa majeshi yake yamepoteza udhibiti kamili wa vijiji viwili vya kaskazini na mashariki mwa Lyman, wakiiacha ngome ya jeshi “ikiwa nusu yake imezingirwa.”

Kushindwa katika eneo hilo kutatoa fursa kwa Ukraine kurejesha ardhi kadhaa ambazo Russia hivi sasa inazishikilia.

Zelenskyy alitangaza mapema Ijumaa kuwa anapeleka maombi ya “haraka” kwa ajili ya kujiunga na NATO.

Marekani imelaani kitendo cha Russia kukamata ardhi. Katika taarifa yake, Rais Joe Biden ameuita ukamataji huo ni wizi.

“Russia inakiuka sheria za kimataifa, inavunja Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kuonyesha dharau kwa amani ya kimataifa kila pahali,” Biden alisema.

Marekani imetangaza vikwazo vingine vipya Ijumaa kwa mamia ya makampuni ya Russia na mtu mmoja mmoja.

Baadhi ya taarifa hii chanzo chake ni mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters

XS
SM
MD
LG