Sherehe hiyo ni juhudi za Kremlin kuhalalisha kile ambacho wengi wanakiona kama hatua isiyo halali kwa matamasha ya sherehe na mikutano ya hadhara huko Moscow.
Kabla ya sherehe hiy kufanyika msafara wa misaada ya kibinadamu ukishambuliwa na makombora ya Russia karibu na mji wa Zaporizhzhia.
Maafisa wanasema takriban watu 23 waliuawawa katika tukio hilo na watu wengine 28 walijeruhiwa. Msafara huo ulielekea katika mji huo ili kuwaokoa wanafamilia kutoka jimbo linalokaliwa.
Wakati huo huo, Finland ndio nchi ya hivi karibuni kufunga mpaka wake kwa Warusi hii leo. Kufungwa kwa mpaka wa Finland kunafanyika wakati kundi la watu kutoka Russia likiendelea kuondoka nchini humo wakitoroka zowezi la kuwaandikisha wanajeshi kwa wanajeshi wapye ili kuendelea na uvamizi wa Ukraine. Aidha, Russia imeanza kufungua ofisi za kutafuta watu katika mipaka yake ili kuwazuia wanaume ambao huenda wanaondoka nchini humo ili kuepuka uhamasishaji huo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilaani vikali unyakuzi huo uliopangwa, akisema ni kinyume cha sheria na lazima ukataliwe.