Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:05

EU kuiwekea vikwazo zaidi Russia kwa "kufanya kura haramu ya maoni" nchini Ukraine


PICHA YA MAKTABA: Rais wa Jumuiya ya Ulaya Ursula von der Leyen
PICHA YA MAKTABA: Rais wa Jumuiya ya Ulaya Ursula von der Leyen

Umoja wa Ulaya umesema kwamba utawawekea vikwazo waandaaji wa kile ulichokiita kura haramu za maoni, katika majimbo manne ya Ukraine yanayodhibitiwa na Russia.

Majimbo hayo yanafanya kile Russia inakiita kura za maoni kwa lengo la kujitenga na Ukraine, hatua ambayo imekosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa, hususan mataifa ya magharibi.

Msemaji wa mkuu wa sera za kigeni wa Umoja, Peter Stano amewaambia waandishi wa habari kuwa kutakuwa na hatua zitakazochukuliwa kwa watu wote watakaoshiriki katika mazoezi hayo, ambayo alisema si ya kisheria, ambayo yaliingia siku ya tano na ya mwisho Jumanne.

Mataifa 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya yanatafakari vikwazo vipya dhidi ya Russia kwa kuandaa kura hizo tata.

Katika zoezi hilo la upigaji kura kwa siku tano, watu katika maeneo ya mikoa ya Luhansk, Donetsk na Kherson wametakiwa kuamua kama wanataka kuwa sehemu ya Shirikisho la Russia au la.

Hayo yanajiri huku rais wa Russia akiendelea kukabiliwa na upinzani na shutuma kutoka kwa raia wa nchi yake, baada ya kutangaza mpango wa kuwapeleka wanajeshi wa ziada wapatao laki tatu kupigana nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG