Trump amezuia kuingia kwa wasafiri kutoka mipaka huru ya nchi zinazotumia mkataba wa viza za Schengen lakini haizihusishi Uingereza na Ireland - katika kile alichosema ni hatua "kabambe" zenye juhudi za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa hatarishi.
Umoja wa Ulaya
Lakini viongozi wa EU wanatoa hoja kuwa ushauri wao wa kisayansi unaeleza kuwa katazo la kusafiri haliwezi kuzuia maambukizi wakati virusi hivyo tayari viko takriban duniani kote, na wamelalamika kuwa hawajashauriwa.
"Virusi vya corona ni mgogoro wa kimataifa, na hauishii katika bara moja, na unahitaji ushirikiano zaidi kuliko maamuzi ya nchi moja," Mkuu wa EU Ursula von der Leyen na Charles Michel wamesema.
"The European Union disapproves of the fact that the US decision to impose a travel ban was taken unilaterally and without consultation," the presidents of the European Commission and European Council said.
"EU inapinga hatua ya Marekani kufanya uamuzi yenyewe kuzuia safari kuingia nchini humo bila ya kuwashauri," marais wa Kamisheni ya EU na Baraza la Ulaya wamesema.
"The European Union is taking strong action to limit the spread of the virus," they insisted.
"EU unachukuwa hatua madhubuti kuzuia kuenea kwa virusi hivyo," wamesisitiza.
Katazo la Trump
Marekani Jumanne ilipiga marufuku wasafiri kutoka Ulaya kuingia Marekani kwa muda wa siku 30, kama mbinu mojawapo ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Hatua hiyo imechukuliwa huku maambukizi yakiendelea kuongezeka kote duniani, na baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza maambukizi ya Corona kuwa janga la kimataifa.
Hata hivyo, marufuku hiyo haitahusisha Uingereza ambayo imeripoti visa 460 vya maambukizi ya Corona.
Rais Donald Trump
Rais Donald Trump amesema : "Baada ya kushauriana na wataalam wetu wa ngazi ya juu wa afya, nimeamua kuchuwa hatua kadhaa muhimu kulinda afya na maslahi ya Wamarekani, kuzuia visa vipya vya maambukizi kuingia katika mipaka yetu. Tunapiga marufuku safari kutoka Ulaya kuingia Marekani kwa muda wa siku 30. Amri hii itaanza kutekelezwa Ijumaa usiku."
Amri ya rais inaeleza kwamba wasafriri kutoka nchi 26 za mkataba wa Schengen wamezuiwa. Hii ina maana kwamba nchi nyingine za Ulaya ikiwemo Ireland, hazitaathirika na marufuku hiyo.
Maafisa walikuwa wamesema kwamba hatari ya maambukizi ilikuwa ndogo sana Marekani, lakini hali ya wasiwasi iliongezeka baada ya maambukizi mapya kuripotiwa mapema Machi.
Juhudi za kuzuia maambukizi kuongezeka zinaendelea kuchukuliwa, ikiwa pamoja na wanajeshi kutumwa New Rochelle, kaskazini mwa mji wa New York, ambapo mlipuko wa Corona nchini Marekani unaaminika kuanzia.
Kikosi cha ulinzi wa taifa kitawapa chakula baadhi ya watu ambao wameambiwa kujitenga na kukaa nyumbani kwao katika sehemu hiyo.
Tangazo la Janga la Kimataifa
Mapema Jumatano WHO lilitangaza mlipuko wa Corona kuwa janga la kimataifa, ikimaanisha ugonjwa huo unasambaa kwa kasi kubwa kote duniani.
Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kiwango cha maambukizi nje ya China imeongezeka mara 13 zaidi katika kipindi cha wiki mbili.
Amesema ana wasiwasi mkubwa na kiwango cha juu cha maambukizi hayo.
WHO imekuwa likifuatilia mlipuko wa Corona kila saa na tuna wasiwasi mkubwa na kiwango cha juu cha maambukizi yanayo endelea kutokea. Kwa sababu hiyo, tunatangaza virusi vya Corona kuwa janga la kimataifa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.