Poland, Estonia, Latvia na Lithuania zilifunga mipaka yao mapema mwezi huu kwa watalii kutoka Russia.
Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Finland amesema kwamba watu kutoka Russia wanaruhusiwa kutembelea familia zao au kufanya kazi au kwa ajili ya masomo.
Hatua ya Finland imejiri baada ya idadi ya raia wa Russia wanaovuka mpaka na kuingia nchi Jirani kuongezeka kwa kazi sana baada ya rais wa Russia kuagiza raia kujiunga na jeshi ili kuendelea kupigana nchini Ukraine.
Putin ametangaza kutuma wanajeshi 300,000 wa akiba nchini Ukriane.
Foleni ndefu zinaenelea kuonekana mpakani, raia wa Russia wakikimbia nchi yao. Foleni pia zinaonekana kuingia Georgia ambayo haihitaji wasafiri kuwa na visa kuingia mipaka yake.