Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:51

Marekani yawataka raia wake kuondoka haraka Russia


FILE - Polisi wa kuzuia ghasia wakimkamata muandamanaji wakati wa maandamano ya kupiga uandikishaji wa nguvu wa raia kutumikia jeshi, Moscow, Russia, Jumatano, Sept. 21, 2022.
FILE - Polisi wa kuzuia ghasia wakimkamata muandamanaji wakati wa maandamano ya kupiga uandikishaji wa nguvu wa raia kutumikia jeshi, Moscow, Russia, Jumatano, Sept. 21, 2022.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeeleza wasiwasi wake Jumatano kuwa Wamarekani wenye uraia pacha na Russia wanaweza kuandikishwa kwa nguvu kusaidia vita vyake dhidi ya Ukraine.

“Russia inaweza kukataa kutambua uraia pacha wa Wamarekani, kuwazuilia kupata msaada kutoka ubalozi mdogo wa Marekani, kuwazuilia kuondoka Russia, na kuwalazimisha wenye uraia pacha kutumikia jeshi,” Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake.

Ilisema kwa kirefu zaidi kuwa raia wa Marekani wasisafiri kwenda Russia na kuwa yeyote aliyeko huko hivi sasa “aondoke Russia mara moja wakati fursa za safari za ndege za abiria zikiwa chache.”

Wizara ya Mambo ya Nje ilisema ndege za abiria kutoka Russia “ni chache mno hivi sasa na aghlabu zinakosekana kwa taarifa fupi. Njia za usafiri wa barabara kwa magari na mabasi bado ziko wazi.”

Lakini imesema Wamarekani wanaosafiri nchini Russia au Wamarekani wanaoishi huko ambao wanapanga kuondoka “wafanye maandalizi yao wenyewe kwa haraka.

Ubalozi wa Marekani umebanwa sana katika uwezo wake wa kuwasaidia raia wa Marekani, na hali, ikiwemo fursa za usafiri wa aina mbalimbali, unaweza kwa ghafla ukazidi kukosekana zaidi.”

Zaidi ya hilo, Wizara ya Mambo ya Nje imewatahadharisha Wamarekani “kuwa haki ya kukusanyika wa amani na uhuru wa kujielezea hauko Russia.

Jiepushe na maandamano ya kisiasa na kujamii na usiwapige picha maafisa wa usalama katika matukio haya. Mamlaka nchini Russia wamewakamata raia wa Marekani walioshiriki katika maandamano.”

XS
SM
MD
LG