Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 11:34

Tume ya uchunguzi ya UN yathibitisha kufanyika kwa uhalifu wa kivita Ukraine


Mwenyekiti wa tume huru ya uchunguzi kuhusu Ukraine, Erik Mose akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya kutoa ripoti kwa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa mjini Geneva, Septemba 23, 2023.
Mwenyekiti wa tume huru ya uchunguzi kuhusu Ukraine, Erik Mose akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya kutoa ripoti kwa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa mjini Geneva, Septemba 23, 2023.

Mwenyekiti wa tume huru ya uchunguzi kuhusu Ukraine amesema leo Ijumaa kwamba, tume hiyo imethibitisha kuwa uhalifu wa kivita ulitendwa nchini Ukraine kufuatia uchunguzi uliofanywa katika mikoa minne ya nchi hiyo.

Erik Mose ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, kwamba "kulingana na ushahidi uliokusanywa na tume, imethibitishwa kuwa uhalifu wa kivita ulitendwa nchini Ukraine,” .

Hakufafanua ni nani waliofanya uhalifu huo lakini kazi ya tume hiyo ilijikita kwenye mikoa ambayo ilikaliwa kimabavu hapo awali na wanajeshi wa Russia kama vile Kyiv, Chernihiv, Kharkiv na Sumy.

Russia ilitakiwa kujibu madai hayo kwenye mkutano wa Baraza hilo, lakini mwakilishi wake hakuwepo kwenye kikao hicho.

Russia imekuwa ikikanusha mara kwa mara kwamba inawashambulia kwa makusudi raia wakati wa kile ilichokiita “operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine na ilisema hapo nyuma kwamba shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu ni kampeni ya kuichafua.

Wachunguzi wa tume hiyo ambayo iliundwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwaka huu, walitembelea maeneo 27 na kuwahoji zaidi ya waathirika 150 na mashahidi.

XS
SM
MD
LG